Saturday, 24 February 2018

Ngoma ‘Kibenten’ yampa usumbufu Beka Flavour

Msanii wa muziki Bongo, Beka Flavour amekiri kupata usumbufu mara baada ya kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Kibenten.
Muimbaji huyo ameiambia The Playlist ya Times Fm kuna baadhi ya watu wamedhani kuwa wimbo huo ulitungwa kuwalenga wao moja kwa moja kitu ambacho si kweli.
“Watu wanasema mwana anatuharibia michongo kwa sababu napata simu mbili tatu, bwana mwanangu mbona unatuharibia, halafu kuna wengine hawasikilizi ngoma vizuri, kwa hiyo mimi sijawasema ila tujiongeze, tujaribu kusikiliza,” amesema Beka.
Ameongeza kuwa wimbo huo hajaimba kwa ajili ya wanaume pekee bali hata wanawake unawahusu kwani hata wao hupitia changamoto kama hizo, hivyo alichofanya yeye ni kutoa elimu.

No comments:

Post a Comment