Monday, 19 February 2018

Mtumishi wa TRA akamatwa kwa kulawiti mtoto

Mtumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Hassan Abuutwalib maarufu Kiringo anashikiliwa na Jeshi la Polisi Zanzibar kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 13.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Hassan Nassir Ali amesema wamemkamata Februari 18, 2018 katika maeneo ya Uwanja wa Ndege Zanzibar alipokuwa akijaribu kuondokea Mwanza.

Kamanda Nassir amesema Kiringo anatuhumiwa kumlawiti mtoto wa miaka 13 baada ya baba wa mtoto huyo jina limehifadhiwa mwenye miaka 54 kuripoti polisi kuwa mtoto wake alichukuliwa na Kiringo na kumpeleka katika nyumba iliyokuwa haijamalizwa kujengwa huko Fuoni Uwandani ambapo alimlawiti baada ya kumpa dawa za kupoteza fahamu na kumsababishia maumivu makali ambapo ripoti ya uchunguzi wa madaktari ilithibitisha kuathirika sehemu za siri za nyuma za mtoto huyo.

Aidha, Kamanda Nasiri amesema ameunda timu ya uchunguzi iliyojumuisha wakuu wa upelelezi wa wilaya tatu Wilaya ya Mjini, Wilaya ya Magharibi A na B kufanya uchunguzi juu ya suala hilo zito ambalo ameshindwa kulifumbia macho.

Kiringo aliwahi kushutumiwa kwa matukio tofauti ya kulawiti kabla ya tukio hili, wananchi wamekuwa wakipiga kelele kwa kuwaharibia vijana wao.

Februari Mwaka 2012, wazanzibari waliwahi kumlalamikia kwa Vyombo vya Dola kwa vitendo vyake hivi:

Hassan Aboud Talib umaarufu Hassan Kiringo, kijana ni mmoja katika vijana wenye akili ya kuzaliwa, baba yake alikuwa ni waziri kiongozi katika awamu ya pili wakati wa uongozi Aboud Jumbe. Huyu ni kijana aliyekulia Michenzani jumba nambari tano, alisoma shule ya Vikokotoni, kwa wakati ule ndie aliyekuwa mwanafunzi aliyepasi vizuri kwa Unguja na Pemba katika kidato cha tatu ndiye alikuwa mwanafunzi bora, na kuendelea na masomo yake shule ya Lumumba na kupata divison 1. Alisoma PCM form six na hatimaye kufutiwa matokeo yake.

Tunayaandika haya na kumtaja Kiringo kwa kutoa mfano wa jamii yetu ilivyoharibika. Huyu ni mfanyakazi wa Idara ya Mapato kwa hiyo shughuli ya pesa kwake sio kubwa kwani kuchota fedha ya serikali sio tatizo kubwa kwake. Ilifikia wakati alikuwa akiwanunulia vijana hadi vespa na kuwanunulia na kumwaga fedha za kiwango cha juu ili apate analolitaka kuwalawiti vijana hao.

Je, kweli nani asiyemjua Kiringo kuwa alikuwa anakaa kinyumba na mtoto wa kiume kama mkewe pale jumba nambari nne Michenzani? Je, kweli hakuna anayeliona hili? Na je hujawahi watu kumuona wanachanganyikana nae maskani au sehemu nyingine?

Hivyo, kweli mtu kama huyu na wenzake wengine ambao wao wamekataa kata kata umbile bora la kike aliloumba Allah na kuchukuwa wanaume na kufata kaumu ya Luti? Lakini kwa vile sisi tumeona ni maendeleo basi tunakaa pembeni na kuyatizama haya. Je, jiulize kweli kwa hali hii umasikini, ufukara na shida zitaondoka visiwani?

Na huyu ni mmoja tu kati ya wengi, kuna Ahmada ambae mkaazi wa Majestic Vuga nyuma pale ya Cinema yeye ndie aliemharibu marehemu Omar Kopa mpaka wakati wa kifo chake, je hili lilikuwa halionekani? Na ilikuwa ukipita Majestic watu wanakaa nae na kufurahi nae na baada ya hapo unaelekea msikitini kusali, je nani unamdanganya?Unamdanganya Allah au unaidanganya nafsi yako
.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: