Monday, 19 February 2018

Mbaroni kwa kuvamia kituo cha polisiWatu wawili wamekamatwa na wengine wawili wakidaiwa kutoroka baada ya Jeshi la Polisi wilayani Ruangwa mkoani Lindi kufanikiwa kuwatia mbaroni kwa madai ya kutaka kuvamia kituo cha polisi wilayani humo huku wakiwa na silaha za kivita.
Kamanda wa Polisi mkoani Lindi, Renatha Mzinga amesema kwa sasa watu hao wako chini ya ulinzi na wanaendelea kuhojiwa.
Amefafanua kwamba “Watuhumiwa hao walikuwa wakizunguka kituo cha polisi kabla ya kudhibitiwa na baadaye kufuatiliwa na kukutwa na zana hizo mbalimbali za uhalifu.” Kamanda Mzinga.
Pamoja na hayo imebainishwa kwamba katika msako ulioendeshwa wilayani Liwale, Polisi wamefanikiwa kukamata silaha ikiwemo bunduki moja ya SMG na mapanga matatu pamoja na vifaa mbalimbali vya kuvunjia sanjari na risasi.
Hata hivyo Jeshi la polisi mkoani Lindi limeendelea kuitahadharisha jamii kutojihusisha na masuala ya  uhalifu huku ikiwekw wazi kwamba taarifa kamili juu ya watuhumiwa itatolewa baada ya kukamilika kwa upelelezi.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: