Thursday, 15 February 2018

Mabeyo aweka wazi hofu aliyokuwa nayo Ikulu leo


Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (CDF), Jenerali Venance Mabeyo amefunguka na kuweka wazi kuwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameweka historia katika jeshi hilo toka kuanzishwa kwake kwa Mkuu wa Majeshi kuwavisha vyeo maafisa wakuu akiwa Ikulu. 

Jenerali Venance Mabeyo amesema hayo leo Februari 15, 2018 wakati Rais Magufuli akimuapisha Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luten Jenerali Yakubu Hassan Mohamed Ikulu Dar es Salaam na kusema yeye amekuwa Mkuu wa Majeshi wa kwanza kufanya zoezi hilo akiwa Ikulu na kusema yeye mwenyewe lilimpa hofu kidogo.

"Naomba nikushukuru wewe Mhe Rais kwa kutualika Ikulu, leo hii katika historia ya jeshi letu ambapo Mkuu wa Majeshi kwa mara ya kwanza kuwavisha vyeo maafisa wakuu wa jeshi akiwa hapa hapa Ikulu, nilikuwa na hofu kidogo maanake naweza mimi nikafikiriwa ndiye Rais sasa nawavisha watu vyeo Ikulu lakini Mhe. Rais nashukuru kwa heshima uliyonipatia kama Mkuu wa Majeshi kama ulivyoniambia jana kuwa Ikulu ni yetu tusiiogope sana" 

Aidha Mabeyo alimshukuru Rais Magufuli kwa kuweza kuwapandisha vyeo kuanzia Mnadhimu Mkuu, Luten Jenerali Yakubu Hassan Mohame na Majenerali Jacob Gidion Kingu, Martin.S.Busungu, Alfred Fabian Kapinga, Kesi Philip Njelekela 

Wengine Rais aliowapandisha vyeo ni, Anselmo Shigongo Bahati, Methiew Edward Mkingule, Blasius Kalima Masanja, Ramadhani.R.Mrangira, Shija Seifu Makona na George Thomas Msongole.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: