TIMU ya Kagera Sugar imelazimishwa sare ya 1-1 na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

Matokeo hayo yanaiongezea pointi moja Azam FC na kufikisha 34 sawa na mabingwa watetezi, Yanga SC ambao hata hivyo wana mchezo mmoja mkononi.

Kagera Sugar yenyewe inafikisha pointi 14 baada ya kucheza mechi 18 na sasa inajinasua mkiani ikirudi nafasi ya 15 kwa wastani wa mabao tu baada ya kulingana kwa pointi na Njombe Mji FC.

Katika mchezo wa leo, Kagera Sugar walitangulia kwa bao la beki Eladslaus Mfulebe dakika ya 50, kabla ya Iddi Kipagwile kuisawazishia Azam FC dakika ya 53.

Kikosi cha Kagera Sugar kilikuwa; Ramadhani Mohammed, Mwaita Gereza, Eladslaus Mfulebe, Juma Shemvuni, Mohammed Faki, George Kavila/Peter Mwalyanzi dk57, Suleiman Mangoma, Ally Nasoro ‘Ufudu’, Japhary Kibaya/Edward Christopher dk79, Ally Ramadhani na Venance Ludovic/Atupele Green dk69.

Azam FC Razack Abalora, Saleh Abdallah/Iddi Kipagwile dk46, Bruce Kangwa, David Mwantika, Yakub Mohammed, Abdallah Kheri, Stephan Kingue/Paul Peter dk74, Frank Domayo, Salmin Hoza, Mbaraka Yussuph/Ennok Atta Agyei dk46 na Shaaban Idd.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: