Shirikisho la mpira wa miguu Africa (CAF) limewataja waamuzi kutoka Burundi kuwa ndio watachezesha mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika kati ya Yanga dhidi ya Township Rollers FC ya Botswana utakaochezwa Machi 6, 2018 kwenye uwanja wa Taifa saa 10:30 jioni.

Mwamuzi wa kati atakuwa Pacifique Ndabihawenimana akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Willy Habimana na mwamuzi msaidizi namba mbili Pascal Ndimunzigo wakati Kamishna wa mchezo huo anatoka Swaziland Mangaluso Jabulani Langwenya

Mechi ya marudiano itachezwa Machin 17, 2018 nchini Botswana na itachezeshwa na waamuzi kutoka Morocco.

Mwamuzi wa kati atakuwa Redouane Jiyed akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Youssef Mabrouk na mwamuzi msaidizi namba mbili Hicham Ait Abou, mwamuzi wa akiba Samir Guezzaz na kamishna wa mchezo huo anatoka Afrika Kusini Gay Makoena
Share To:

msumbanews

Post A Comment: