Thursday, 22 February 2018

HALMASHAURI ZOTE TANZANIA ZATAKIWA KUIGA MFANO WA HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA KATIKA KUKUZA MAENDELEO YA NCHI.

Bi Tajiel Mahega Mratibu wa TASAF jiji la Arusha akisoma ripoti ya ujenzi wa vyumba vya mdarasa pamoja na ujenzi wa vyoo mbele ya mgani rasmi.

Na Lucas Myovela

Hayo yamesema na katibu mwenezi wa Ccm taifa Humphrey Polepole wakati wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano pamoja na miradi ya wananchi iliyopo chini ya TASAF jiji la Arusha wenye mpango wa kunusuru kaya maskini.

Polepole amesema hayo akiwa katika ukaguzi wa kituo cha afya kilichopo katika kata ya Murriet  kinacho jengwa na serikali kupitia halmashauri ya jiji la Arusha chini ya usimamizi wa mkurugenzi wa jiji la Arusha Athuman Kihamia,ujenzi huo huo utakao gharimu shilingi Bilioni 1.2 hadi kukamilika kwa kituo hicho cha Afya  na mpaka sasa katika ujenzi wa awali wa kituo hicho kimesha gharimu zaidi ya milioni 280.

"Nikiwa kama katibu wa itikadi na uwenezi ngazi ya taifa nataka niwatake wakurugenzi na wakuu wa wilaya wote hapa nchini kuiga mfano wa maendeleo katika jiji la Arusha nimpongeze mkurugenzi wa jiji hili kwa michoro mizuri na ubunifu wa hali ya juu katika kufanya maendeleo ya jiji na wananchi kupata maendeleo na kunufaika na serikali yao huu ndio uongozi tunaoutaka katika serikali ya awamu ya tano pia niwapongeze mkuu wa wilaya hii pamoja na Mkuu wa mkoa huu wa Arusha" Alisema Polepole

Akisoma ripoti ya ujenzi wa hosptali hiyo dactari mkuu wa mkoa Dk Simon Chacha amesema kuwa kituo hicho cha afya kitatoa huduma za wagonjwa wa nje ( OPD ), huduma za upimaji maabara,huduma ya kujifungua,huduma ya uzazi ya mama na mtoto,huduma ya kulaza wagonjwa ( IPD) pamoja na huduma za upasuaji.

Awali Mkurugenzi wa jiji la Arusha Athuman Kihamia akisoma ripoti ya utekelezaji wa miradi iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa na halmashauti ya jiji la Arusha alisema kuwa kufikia maendeleo yenyetija wao kama jiji waliamua kuwatumia mafundi ambao ni chipukizi amabao gharama.zao ni nafuu tofauti na mwanzo ambapo gharama za ujenzi wa maelendeleo zilikuwa ni kubwa na miradi mingi kuishia njiani pasipo kukamilika na hasa katika ujenzi wa madarasa pamoja na madawati.

"Nilipo fika hapa nilikuta darasa moja linajengwa kwa shilingi milioni 34 bila madawati lakini kwa hivi sasa tunajenga dara moja kwa silingi milioni 20 pamoja na madawati yake kwa wanafunzi 45 wa darasa husika na pili tumepunguza matumizi yasiyo na lazima ili fedha hizo ziwanufaishe wananchi na sio kwa mtu mmoja mmoja" Alisema Kihamia.

Nae kwa upande wake mratibu wa Tasaf jiji la Arusha Bi Tajiel Mahenga ambae pia ni msimamizi mkuu wa miradi ya maendeleo ya  TASAF jiji la Arusha amesema kuwa jiji la Arusha limefanya uhawilishaji wa fedha kwa kaya maskini 1484 na mifugo mbali mbali kwa baadhi ya kaya kama njia ya ujasiliamali na vitega uchumi huku kaya 3563 zimeshapokea malipo taslimu yenye jumla ya shilingi 139,606,950 kwa mitaa yote 70 ya jiji la Arusha na malipo ya yaliyo lipo kwa njia ya mtandao kwa kaya 62 ni jumla shilingi 22,391,300 katika kipindi kimoja cha malipo.

Aidha pia Mahenga amesema kuwa TASAF imeweza kujenga madarasa mawili  kwa gharama ya shilingi 41,579,900 katika shule ya msingi suye na matundu manne ya vyoo kwa  gharama ya shilingi 8,133,700 na ujenzi wa daraja la kivuko cha miguu katika kata ya Olasiti katika mtaa wa  Olelesho ujenzi uliyo gharimu zaidi ya shilingi milioni 49.

Ziara hiyo ya kikazi ya Polepole ya ukaguzi wa miradi inayotekelezwa chini ya ilani ya chama cha mapinzi ccm pia ameweza kutembelea kaya zenye uwezo mdogo katika kata mbali mbali za jiji la Arusha zinazo wezeshwa na TASAF pamoja na kukagua vikundi mbalimbali vya wakina mama waliyo wezeshwa na TASAF huku akipokea wanachama wapya waliyohama kutoka katika  vyama mbali mbali vya siasa na kujiunga na chama cha mapinduzi ccm.

Baadhi ya Picha Mbalimbali kwenye Ziara hiyo.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: