Articles by "UWT"
Showing posts with label UWT. Show all posts

 


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amewataka Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Jumuiya ya CCM, kuendelea kuwa sauti ya wanawake nchini na kuwahamasisha kushiriki siasa, akiwataka wahakikishe wanawafikia watu wote, kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu.


Katika kutimiza jukumu hilo, Balozi Nchimbi amewahimiza UWT kuendelea kuwatembelea wananchi nchi nzima, kama wanavyofanya sasa, kupitia ziara zao, ambazo pia amewaambia waendelee kuzitumia kuyatangaza mafanikio makubwa yaliyofanywa na yanayoendelea kufanywa na Serikali ya CCM, chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Balozi Nchimbi amesema hayo alipokuwa akifungua mafunzo ya afya ya uzazi, mama na mtoto kwa Wajumbe wa Baraza Kuu la UWT, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Dodoma, leo Ijumaa, Agosti 2, 2024,

“Hongereni sana kwa kazi kubwa na nzuri mnayoendelea kuifanya ya kuimarisha Jumuiya. Tumeona amsha amsha yenu mnayofanya kila kona. Hongereni sana pia kwa kuendelea kusajili wanachama wengi. Tunataka muendelee hivyo hivyo kwa vitendo ili muongoze. Na sasa tunaelekea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, msiache ziara za kukutana na wananchi.

“Kwenye CCM wanawake ni jeshi la kutegemewa. UWT hakikisheni watu wote wanafikiwa. Mnao wajibu mkubwa kwa Jumuiya yenu, kwa Chama Cha Mapinduzi na Mwenyekiti wa CCM. Kazi ya kuhamasisha maendeleo na kutangaza mafanikio makubwa kutokana na kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya CCM, chini ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan mkaifanye bila kumuonea haya mtu yeyote,” amesema Balozi Nchimbi.

Naye Mwenyekiti wa UWT Taifa, Ndugu Mary Pius Chatanda, akimkaribisha kuzungumza, ameushukuru uongozi wa Chama kwa jinsi unavyoendelea kuwaamini UWT, na kumuomba Katibu Mkuu Balozi Nchimbi afikishe salaam kwa Mwenyekiti wa CCM kuwa jumuiya hiyo itaendelea kufanya kazi kubwa kwa ajili ya CCM na nchi kwa ujumla, ikiwemo kuendelea kuwahamasisha wanawake kushiriki shughuli za kisiasa nchini.






 


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Ndg. Mary Chatanda kwa kushirikiana na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa serikali wametoa mafunzo maaalum kwa viongozi wanawake kutoka mikoa 9 ya Kanda ya Ziwa na Kanda ya Ziwa Magharibi. Dhima kuu ikiwa ni kuwajengea uwezo Wanawake namna ya kutumia matokeo ya Sensa katika kuchochea maendeleo sanjari na Kuleta ufanisi wa Utendaji wa kazi  katika kujikwamua kiuchumi na kijamii.

Mafunzo hayo ya Siku moja yamehusisha viongozi wanawake pamoja na Waheshimiwa Madiwani Viti Maalum kutoka mikoa ya Mwanza, Kagera, Katavi, Shinyanga, Simiyu, Geita, Kigoma, Tabora pamoja na Mkoa wa Mara leo tarehe 27/3/2024 Katika Ukumbi wa Winterfell  Mkoani Mwanza.

Kadharika mafunzo hayo yamehudhuriwa na Mhe. Anne Makinda Spika Mstaafu wa Bunge La Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kamisaa wa Sensa, Katibu Mkuu wa UWT Ndg. Jokate Mwegelo, Naibu katibu Mkuu UWT Bara Ndg. Riziki Kingwande pamoja na Mhe. Amina Makilagi Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.




 Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT, Mary Chatanda na msafara alioambata nao wamejikuta katika Simanzi nzito mara baada ya kumuona Mama aliyejifungua saa chache mara baada ya kuokolewa kwenye tope ambalo lilikuwa limemuonea mwili mzima na kumsomba mita kadhaa.


Akizungumza leo alipomtembelea Mwanamke huyo katika Kituo cha Afya Gendabi mahali ambapo ndipo kulikuwa na Maafa makubwa kufuatia mafuriko yaliyotokea mara baada ya Mlima Hanang kupasuka.

"Nimeshindwa kujizuia mimi kama Mama nikajikuta nalia kwa uchungu kuona Mwanamama huyu ambaye alisombwa na tope na kuweza kuokolewa kwenye tope hilo na kufikishwa hospital masaa mawili baadaye kujifungua salama

Mtoto wa kiume 3/12/2023 kwa kweli nimelia uchungu baada ya kusikiliza simulizi za Mama huyu namna alivyohangaika kuokoa watoto wake wawili na huku mjamzito wa miezi tisa hakika hakuna kama Mama . Namshukuru sana Mungu kutenda maajabu na kumuwezesha Mama huyu kujifungua salama na mtoto yupo Salama na ameitwa Mussa ."

Aidha Mwenyekiti amesema Jumuiya itafanya jitihada kuhakikisha wanamuongezea mahitaji ya kutosha

Mama huyo ambaye kwa sasa yeye na familia wanalala hospitali kutokana na kukosa Makazi baada ya makazi yao kuharibiwa vibaya kutokana na mafuriko ya matope yaliyoikumba baadhi ya maeneo ya wilaya ya Hanang .





 Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya maafa iliyotokea tarehe 2/12/2023 Wilaya ya Hanang Mkoa wa Manyara kufuatia mvua kubwa iliyopelekea mafuriko na Mawe makubwa na Miti kutoka Mlima Hanang kuporomoka na kuingia mji wa Kateshi na kusababisha athari kwa kaya 1,150 na watu 5,600, na kusababisha  vifo vya watu zaidi ya 50 na majeruhi 80 ambao wamepelekwa hospital mbalimbali.

Natoa  pole kwa Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan,Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,ndugu ,jamaa na marafiki walioguswa na misiba hiyo na nawaombe Marehemu wapumzike mahala pema Peponi na majeruhi wote wapone haraka,pia  natuma salam za pole kwa wananchi wote waliokumbwa na maafa hayo. 

UWT inapongeza Juhudi za Serikali kwa hatua mbalimbali za haraka zilizochukuliwa kutokana na maafa haya,ikiwemo msaada wa dharura  na uokoaji, kuwapatia makazi na kugharamia matibabu kwa waathirika.

Aidha sisi UWT tunaiunga Mkono Serikali kwenye jitihada hizo na leo tarehe 4/12/2023 jiji Dar Es Salaam imefanyika Kamati ya Utekelezaji ya Dharura ambayo imewaalika wajumbe wa Baraza Kuu waliopo Dar Es Saalam,wabunge wa Viti Maalum na baadhi ya viongozi na tumejipanga kwenda Hanang haraka kuwafariji wananchi wenzetu waliofikwa na maafa haya na kwenda kukabidhi vifaa mbalimbali ambavyo UWT kwa kushirikiana na wadau wetu tumefanikiwa kuvinunua ikiwemo; 

Magodoro-100 ,Mashuka -50,Mablangeti -50,Vikoa 500,Madila 520 na vifaa mbalimbali kama vinavyoonekana Kwa kutambua kuwa uhitaji ni mkubwa na kwakuwa waathirika wakubwa kwenye maafa haya ni Wanawake na Watoto UWT tumewaelekeza wabunge wanawake wa CCM waendelea kuchangia kwa UWT ili tuendelee kuongeza vifaa hivi na tunatoa wito wa Wanawake wote kuguswa na kilichotokea Hanang ili waungane na UWT na  tumuunge mkono  Rais wetu Dkt Samia kwa kuwasaidia wananchi wenzetu wa Hanang walikumbwa na maafa.

Pia nawakaribisha wadau mbalimbali wenye nguo na vifaa vingine ambavyo vinaweza kuwa sadaka yako kwa wananchi wenzetu wa hanang, tunawakaribisha sana mziwasilishe kwenye ofisi zetu za UWT Makao Makuu Dodoma,Ofisi ndogo Dar Es Salaam zilizopo ofisi za CCM Mkoa wa Dar Es salaam.






 FATMA REMBO AKABIDHI PIKIPIKI NA TOFARI 1000  KUSUKUMA MAENDELEO YA UWT KATIKA KILA WILAYA YA MKOA WA IRINGA



Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Mkoa wa Iringa Injinia Fatma Rembo ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa UWT Taifa, amekabidhi pikipiki nne kwenye wilaya za mkoa wa Iringa ili kusukuma maendeleo.


Pamoja na pikipiki hizo, amekabidhi Shilingi 1,000,000 kwa wilaya hizo kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa nyumba za makatibu wa jumuiya hiyo.


Wilaya zilizopewa pikipiki hizo ni Mufindi, Kilolo, Iringa Mjini na Iringa Vijijini.


Akikabidhi pikipiki hizo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Comred  Daud Yasin Mlowe amempongeza Injinia Fatma huku akisisitiza suala kila kiongozi kutekeleza wajibu wake.

Comred Yassin amewaomba wazitunze pikipiki hizo ili ziendelee kusaidia kazi mbalimbali na uchumi.


"Tuendelee kumuunga mkono Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kufanya kazi kwa bidii. Tuendelee kumsemea," amesema Comred Yassin.


Injinia Rembo amesema baada ya ziara yake kwenye wilaya zote Mkoani Iringa aliahidi kukabidhi pikipiki na fedha kwa ajili ya matofari.


"Pia tuendelee kumuunga mkono Rais Samia kwa kuchapa kazi na kumsemea mazuri , pikipiki hizi zitatusaidia sana kwenye changamoto za kiuchumie," amesema Rembo.


Awali, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Comred Salim Asas Abri alisisitiza upendo.


"Kina mama mpendane, mkiyumba nyie chama kimeyumba pia, mkiona mwenzio amefanya jema mpongeze. Pia muwe mstari wa mbele kumtetea mwanamama mwenzenu,, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.


Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Iringa, Comred  Zainab Mwamwindi alizungumzia umoja na mshikamano miongoni mwao.


"Nampongeza Fatma na kwa kweli tuendelee kushikamana, tufanye kazi kwa umoja na upendo," amesema Mwamwindi.

 

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uomja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mary Chatanda akipokea kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan  zawadi ya picha ya kuchora ya Rais kutoka kwa Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dodoma, Neema Majule katika mkutano wa kumpongeza  Dkt. Samia kwa ushindi mkubwa alioupata katika uchaguzi wa chama hicho lakini pia kumkaribisha Chatanda.

 Mkutano huo uliofanyika Disemba 9, 2022 kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa UWT na wanachama wa CCM ambapo pia Chatanda na makamu wake Zainab Shomari walizawadiwa zawadi mbalimbali

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama (kushoto) akipokea tuzo kwa niaba ya Rais kutoka kwa Mwenyekiti wa UWT Taifa, Chatanda.

Makundi mbalimbali  yakitoa zawadi kwa Mwenyekiti wa UWT Taifa, Chatanda na Makamu Mwenyekiti Zainab Shomari.