Kariakoo, 11 Septemba, 2026
Wafanyabiashara wa vipodozi katika Mtaa wa Vipodozi Kariakoo, Dar es Salaam, wamepata elimu kuhusu masuala ya kodi na huduma zinazotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kupitia ziara ya maafisa wa mamlaka hiyo iliyoongozwa na Kaimu Meneja wa Mkoa wa Kodi Kariakoo, Edson Issanya.
Katika ziara hiyo, wafanyabiashara walielekezwa kuhusu matumizi sahihi ya mashine za EFD kupitia mfumo mpya wa POS unaounganishwa na mfumo wa IDRAS, pamoja na ulipaji wa kodi ya awamu ya tatu kwa mwezi Septemba.
Aidha, walipatiwa elimu kuhusu mabadiliko ya sheria za kodi kwa mwaka mpya wa fedha, hususan masuala ya misamaha na ahueni za kodi kwa wafanyabiashara wanaokidhi vigezo vilivyowekwa.











Post A Comment: