Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kuhakikisha bei za mafuta nchini zinakuwa himilivu na zinalinda maslahi ya wananchi, ikiwa ni pamoja na kuimarisha usimamizi wa soko na kuhakikisha upatikanaji wa mafuta kwa wakati katika maeneo mbalimbali nchini.

Hatua hizo zimechangia kupunguza athari za mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la dunia.

Kwa mwezi Septemba 2026, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza kushuka kwa bei za mafuta hali inayotarajiwa kuleta unafuu kwa watumiaji.

Bei ya petroli imepungua kwa shilingi 102 kwa lita, huku bei ya dizeli ikishuka kwa shilingi 101 kwa lita.

EWURA imeonya kuwa wauzaji wa mafuta watakaokiuka bei elekezi watachukuliwa hatua kali za kisheria, na kwamba wakaguzi wa Mamlaka hiyo tayari wapo kazini katika maeneo mbali mbali kuhakikisha sheria na taratibu zinafuatwa.

Watumiaji wa mafuta wameshauriwa kuchukua risiti wanaponunua mafuta, kwani nyaraka hizo hutumika kama ushahidi kunapokuwa na changamoto yoyote.

Share To:

Alex Sonna

Post A Comment: