
Na; Mwandishi wetu-Tanga.
Ujumbe kutoka Mfuko wa Kimataifa la Kuendeleza Kilimo (IFAD) na wataalamu kutoka katika sekta zinazotekeleza Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) wamekutana Mkoani Tanga Tarehe 7 Septemba 2026 kwa lengo la kufanya mapitio ya Utekelezaji wa Programu hiyo.
Sambamba na hilo timu hiyo itatembelea maeneo yanayotekeleza Programu kwa Mkoa wa Tanga, ambapo kwa upande wa sekta ya kilimo timu hiyo itatembelea kata ya Msomela iliyopo katika Halmashauri ya Handeni Vijijini ambako programu imehamasisha na kutoa elimu ya kilimo bora kwa jamii ya kimasai ambao kiasili ni wafugaji ambapo wameweza kujishughulisha na kilimo cha mahindi chenye tija.

Programu imewezesha kuwepo kwa eneo la mashamba darasa (FFS) kwa mazao ya Alizeti, Mahindi na Maharage, na shamba Darasa hilo limeonesha mafanikio kwa kiasi kikubwa, ambapo hekta moja inaweza kuzalisha takribani magunia 20 ya kilo mia moja kila moja, na jamii ya wafugaji sasa inajishulisha na shughuli za Kilimo na kunufaika na upatikanaji wa mazao yanayolimwa.

Kwa upande wa Sekta ya Uvuvi, Programu inaendelea na ujenzi wa soko la kimataifa la Samaki Kipumbwi lililloko katika halmashauri ya Pangani ambapo mpaka sasa ujenzi umefikia asilimia 68% na linategemewa kukamilika ifikapo Oktoba 2026.
Aidha, programu pia inaendelea na ujenzi wa vichanja 40 vya kukaushia dagaa ambavyo vinaweza kukausha takribani tani tano kwa za dagaa kwa wakati mmoja.

Kwa upande mwingine pia Programu ya AFDP inaendelea na ujenzi wa Ghala la baridi na mtambo wa barafu katika soko hilo kwa ajili ya kuhifadhi na kusafirisha samaki.

Awali Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la kimataifa la maendeleo ya Kilimo nchini (IFAD) Bw. Seth Meng alikutana na Kaimu Katibu tawala wa Mkoa wa Tanga Bw.Emmanuel Kisongo na kufanya mazungumzo kuhusiana na utekelezaji wa Programu katika Mkoa sambamba na mafanikio tarajiwa kwa wanachi wa maeneo husika ambapo Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa alieleza kuwa Programu hiyo ni muhimu sana katika kuhamasisha maendeleo ya kilimo na uvuvi katika mkoa huo.
hi Aliishukuru IFAD kwa kuweza kuwafikia wananchi wa mkoa huo na kuwataka ikiwezekana kuongeza uwekezaji mkoani hapo.
Post A Comment: