Na William Bundala-Kahama Shinyanga

Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika kata ya Majengo manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga imeishukuru na kuipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha zaidi ya Shilingi milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu ya barabara katika kata hiyo.

Hayo yamebainishwa leo katika ziara ya kutembelea na kukagua ujenzi wa barabara za mtaa wa Sokola na majani mapana ambazo zinawekewa mitaro na kukwanguliwa kwa kiwango cha moramu.

Akiongea katika ziara hiyo Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi kata ya Maajengo Noel Mseveni amesema kuwa wamejionea utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi na amepongeza Mh Diwani wa kata hiyo Zacharia Soko kwa kupambania maendeleo ya kata ya majengo kwa kuisemea kata na kutumia fedha zake binafsi.

“Sisi kama chama tunashukuru sana na kuipongeza serikali yetu Sikivu kwa kutupatia fedha nyingi za ukarabati wa miundo mbinu ya barabara katika kata yetu,pia tunampongeze sana diwani wetu soko kwa kujitolea katika shughuli mbalimbali za maendeleo kwa gharama zake” Amesema Mseveni.

Nao wajumbe wa kamati ya siasa akiwemo Mariam Visent,Amani Kibela ana Saimoni Patrick wamesema kuwa barabara nyingi za mitaa ya majengo zilikuwa hazipitika kwa muda mrefu lakini kwa sasa mitaa mingi imefunguka na barabara zinapitika na kutoa pongezi kwa diwani wa kata hiyo Zacharia Soko kwa juhudi zake za kupambania ukarabati wa barabara.

“Barabara zetu zilikuwa hazipitiki kwa muda mrefu sana lakini kwa sasa tunamshukuru Rais Samia na jitihada za diwani wetu kwa kuhakikisha wana majengo wanarudisha tabasamu kupitia barabara zetu,sasa hivi hata bodaboda zinafika hadi mlangoni tofauti za zamani” Wamesema wajumbe hao.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Majengo Zacharia Soko amesema kuwa ataendelea kuziunganisha barabara zote za mitaa ya majengo na kwamba ataisimamia ilani ya chama cha Mapinduzi kama alivyoagizwa na chama na amekabidhi katapila kwa mwenyekiti wa mtaa wa Majengo Patroba Ndambigeze ili akasimamie ukarabati wa barabara za mtaa wa Sokola.

“Naishukuru sana serikali yetu kwa kutupatia fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa barabara,mimi nimeunga mkono serikali yangu kwa kutoa shilingi milioni kumi na saba kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za serikali katika ujenzi wa barabara,nakuomba sana mwenyekiti nakukabidhi katapila hili nenda ukasimamie ujenzi wa barabara za mtaa wa Sokola ka kiwango kinachotakiwa” Amesema Soko.

Awali akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa barabara hizo injiania wa wakala wa barabara za vijijini na mijini (TARURA) Shija Mhangale amesema kuwa kata ya majengo ina miradi miwili ya barabara na kwamba ujenzi wa barabara hizo utakamilika mwishoni mwa mwezi huu.

“Kata ya majengo ina miradi miwili ya ujenzi wa barabara ambazo ni barabara ya majani mapana na barabara ya Majengo Nyanshimbi,na shughuli zinazofanywa katika miradi hii ni kujenga barabara na mitalo Pamoja na madaraja,hivyo ka kasi ya mkandarasi tunatarajia kukamilisha ujenzi mwishoni mwa mwezi huu” Amesema Shija.
Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

OSCAR ASSENGA

Post A Comment: