Julai 14, 2026 - Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Eliakim Maswi leo amekutana na wajumbe wa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NaCoNGO )pamoja na wawakilishi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ngazi za mikoa na wilaya.

Lengo la kikao hicho ni kujadili kwa pamoja utekelezaji wa Dira 2050 kupitia Sekta imara ya NGOs, ambapo Maswi amesisitiza kuwa na ushirikiano wa kimkakati unaoweza kuleta mabadiliko chanya kwani Wizara na Mashirika ndiyo ustawi wa jamii.

Aidha, Maswi ametoa wito kuwa Taifa halijengwi kwa nguvu au mabavu, taifa linajengwa kwa kushirikiana. Safari ya Utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya 2025 bila NGO’s itakuwa ngumu, ameahidi kuwa Serikali inatoka kwenye udhibiti na kujenga ushirikiano wa kimkakati ili kutengeneza timu ya ushindi.
Share To:

OSCAR ASSENGA

Post A Comment: