Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, George Masaju, akiwasilisha hotuba yake ya ufunguzi wa mafunzo ya usalama na afya kazini ya siku mbili (Julai 2-3, 2026) yanayotolewa na OSHA kwa Majaji wa Mahakama ya Rufani na Viongozi Waandamiziwa Mahakama.
**************
Na Mwandishi Wetu
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, George Masaju, ameshauri Wakala wa Usalamana Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kuendelea kufanya ukaguzi wa mifumo ya usalama na afya katika maeneo ya kazi nchini yakiwemo majengo ya Mahakama kwa mujibu wa Sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi, Sura Na. 297, Marejeo ya 2023.
Ametoa kauli hiyo Jijini Dodoma katika hotuba yake ya ufunguzi wa mafunzo ya usalama na afya kazini ya siku mbili (Julai 2-3, 2026) yanayotolewa na OSHA kwa Majaji wa Mahakama ya Rufani na Viongozi Waandamizi wa Mahakama.
Lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwajengea uelewa viongozi hao wa Mhimili wa Mahakama ambao baadhi yao wameteuliwa hivi karibuni ili waweze kutekeleza majukumu yao ya msingi kwa kuzingatia viwango stahiki vya usalama na afya kwa mustakabali mzima wa afya, usalama, ustawi na maendeleo ya Taifa.
Jaji Mkuu amesema msingi wa Sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ni Katiba yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania hususan Ibara ya 12 na 14 zinazosisitiza juu ya umuhimu wa kulinda haki na utu wa watu.
“Kazi tunazozifanya hazipaswa kuhatarisha maisha yetu kwa namna yoyote ile nakimsingi tunafanya kazi kwa lengo ya kujiletea maendeleo ambayo kimantiki yanapangwa nasisi wenyewe ili yatusaidie sisi wenyewe hivyo ili kufaidi matunda yamaendeleo tunayoyatafuta hatuna budi kulinda afya zetu,” ameeleza Jaji Mkuu.
Aidha, ameeleza kwamba mafunzo mbalimbali yakiwemo yanayohusu usalama na afyakazini ni muhimu kwa watumishi wa Mahakama na makundi mengine katika jamii kama ilivyoainishwa katika Dira ya Taifa 2050 katika nguzo ya pili inayosisitiza juu ya uhitajiwa kujenga uwezo wa watu na jamii unaojumuisha ujuzi, stadi za maisha, uhuru wakuchagua na kufanya maamuzi, pamoja na fursa zilizopo zinazomwezesha kila mtukuishi maisha bora.
“Ili tuweze kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuimarisha mfumo wa utoaji haki na utawala bora nchini ni lazima tuhakikishe kwamba rasimali watu ya Mahakama inalindwa kupitia uboreshaji wa mazingira, miundombinu na kuiwezesha kupitia mafunzo kama haya,” amesema Jaji Mkuu Masaju.
Akitoa salamu za awali katika ufunguzi wa mafunzo hayo, Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, amesema Mahakama ni mdau muhimu katika kusimamia utekelezajiwa Sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi na kwamba ni muhimu kuhakikisha kwamba kunakuwa na uelewa wa pamoja juu ya usimamizi masuala ya usalama naafya nchini baina ya OSHA na watendaji na viongozi wa Mahakama.
Amesema Taasisi ya OSHA itaendelea kushirikiana na Mahakama kupitia programu za mafunzo na uchunguzi wa afya za watendaji na viongozi wa Mahakama katika ngazi mbalimbali pamoja na kuhakikisha kwamba miundombinu ya Mahakama inafanyiwa ukaguzi ili kuhakikisha kwamba inakidhi viwango stahiki vya usalama na afya mahali pa kazi.
OSHA emekuwa ikitoa mafunzo ya usalama na afya kwa watendaji na viongozi wa Mahakama katika ngazi mbalimbali kwa awamu tofauti ikiwa ni utekelezaji wa mkakatiwa Taasisi wa kuyafikia makundi mbalimbali ya wadau. Awamu hii inawahusu Majaji 24 wa Mahakama ya Rufani pamoja na Viongozi Waandamizi wa Mahakama ambao sambamba na kupatiwa mafunzo, wamekabidhiwa vifaa muhimu vikiwemo viti vya igonomia na masanduku ya huduma ya kwanza.
Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, akitoa salamu za awali katika ufunguzi wa mafunzo ya usalama na afya kazini ya siku mbili (Julai 2-3, 2026) yanayotolewa na OSHA kwa Majaji wa Mahakama ya Rufani na Viongozi Waandamizi wa Mahakama.
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, George Masaju, akikabidhiwa sanduku la huduma ya kwanza likiwa ni miongoni mwa vifaa vilivyotolewa na OSHA sambamba na mafunzo ya usalama na afya kazini kwa Majaji wa Mahakama ya Rufani na Viongozi Waandamizi wa Mahakama.
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, George Masaju na Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda wakiwa wameshika kiti cha igonomia ambacho ni mfano wa viti 22 vitakavyotolewa na OSHA kwa Majaji 22 wa Mahakama ya Rufani ikiwa ni sehemu ya uhamasishaji uzingatiaji kanuni bora za igonomia kwa wafanyakazi ambao shughuli zaozinawataka kukaa ofisini kwa muda mrefu.









Post A Comment: