Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) ambaye pia ni mratibu wa kitaifa wa mtandao wa kuzuia na kupambana na majanga ya kikemia, kibaolojia, kiradiolojia na kinyuklia (CBRN) Prof. NAJAT KASSIM MOHAMMED amesema elimu ya kupambana na majanga itaanza kutolewa kupitia vyombo vya habari ili kuwapa wananchi uelewa wa namna ya kuwa tayari kukabiliana na majanga mbalimbali.
Prof. NAJAT ameyasema hayo jijini Dodoma wakati wa kikao cha kamati ya kitaifa ya kupambana na majanga ya kikemia, kibaolojia, kiradiolojia na kinyuklia (CBRN) ikiwa ni maelekezo yaliyotolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ya kuitaka kamati hiyo kuhakikisha wananchi wanapewa elimu ya majanga mbalimbali na namna ya kukabiliana na dharura.
Afisa Mkaguzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha menejimenti ya maafa Bwn. PASCAL KANILE amesema umuhimu wa kikao hicho ni kuhakikisha kila taasisi iliyolengwa inawajibika katika kuandaa wataalamu wake kuwa tayari kukabiliana na majanga.
Kwa upande wake mwakilishi kutoka Kamisheni ya kukabilianba na maafa Zanzibar Bwn. SAID CHANDE SAID amesema kutokana na maendeleo ya shughuli za binadamu ni muda sahihi wa kuwa na utayari wa kukabiliana na dharura yoyote inapojitokeza.
Wakati wa uzinduzi wa zoezi la utayari dhidi ya dharura za kikemikali ,kibaolojia, kiradiolojia na kinyuklia (ZOKIKITA) Mwezi Machi 2024, Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA alitoa maelekezo kwa kamati ya kitaifa kuhakiksha wanakutana na kujengeana uwezo wa kuhakikisha nchi inakuwa na utayari wa kukabiliana na dharura.
Post A Comment: