Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda ameyakaribisha mashirika na asasi za kiraia zilipo mkoani Arusha, kuweza kushirikiana na ofisi yake na ofisi nyingine za Umma zilizopo mkoani hapa ili kuweza kushirikiana na kuongeza kasi zaidi katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Mhe. Makonda ametoa kauli hiyo mapema leo Julai 08, 2024 wakati wa mkutano wake na wadau wa mashirika na asasi hizo zinazoshughulika na maendeleo ya huduma za jamii, mkutano wenye lengo la kufahamiana na kuwasikiliza katika jitihada za kuendelea kuwatumikia wananchi.

"Niwakaribishe kuitumia ofisi ya Mkoa kama sehemu ya ofisi yenu,Jambo lolote unaloweza kuwa nalo, Mtu yeyote mwenye shughuli ndani ya mkoa wa Arusha, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Ofisi ya mkuu wa wilaya ni ofisi yako.Unapaswa kwenda kifua mbele na kuomba mahitaji yako ili ufanikishe kile unachokifanya ambacho sisi tunaamini ndicho kinachoweza kuleta tija kwenye maisha ya wananchi tunaowaongoza." ameongeza Mhe. Makonda.

Katika Mkutano huo wadau wa asasi hizo za kijamii zinazofikia takribani 1224, wanatoa maoni na changamoto zao kwa Mkuu wa Mkoa Mhe. Makonda ambaye ameahidi kuzifanyia kazi katika shabaha ya kuongeza ufanisi na kasi ya utendaji wao wa kazi na kuweka mazingira rafiki ya mashirika hayo katika kuwatumikia wananchi wa Mkoa wa Arusha.
Share To:

Post A Comment: