Mkaguzi msaidizi wa polisi wilaya ya Nachingwea Asha Mponda ambaye ni mkuu wa dawati la jinsia na watoto wilaya ya Nachingwea akiongea na watoto juu ya umuhimu wa kutoa taarifa za vitendo vya ukatili wa kijinsia
Mkaguzi msaidizi wa polisi wilaya ya Nachingwea Asha Mponda ambaye ni mkuu wa dawati la jinsia na watoto wilaya ya Nachingwea akitoa zawadi kwa watoto
Na Fredy Mgunda, Nachingwea.
JESHI la polisi wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi limetoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa zaidi ya watoto 500 ili kuwajengea uwezo wa kutoa taarifa pale wanapoona wanafanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Akizungumza wakati wa kutoa elimu hiyo, mkaguzi msaidizi wa polisi wilaya ya Nachingwea Asha Mponda ambaye ni mkuu wa dawati la jinsia na watoto wilaya ya Nachingwea alisema kuwa kumekuwa na ongezeko la watoto kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia hivyo wameamua kutoa elimu hiyo ili watoto waweze kutoa taarifa za vitendo hivyo.
Mponda alisema kuwa wamekuwa wakitoa elimu ya ukatili wa kijinsia mara kwa mara lakini sasa wameamua kutumia michezo mbalimbali kutoa elimu hiyo ili watoto waweze kujijengea uwezo wa kutoa taarifa.
Alimalizia kwa kuwataka wananchi wa wilaya ya Nachingwea kuachana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa jamii ili kuwa na kizazi bora kwa faida ya taifa na familia zao.
Post A Comment: