Na Denis Chambi, Tanga
JUMLA ya walimu 2000 wa shule za Sekondari za kata katika Mikoa ya Dodoma, Mbeya visiwani Zanzibar wameunganishwa na huduma ya Smart wasomi iliyopo chini ya Kampuni ya Airtel Tanzania wenye lengo la kuwasaidia kupata maudhui ya elimu kwa njia ya mtandao.
Mradi huo ambao umewashirikisha wadau kutoka Shiriki la Umoja wa mataifa la kumhudumia watoto 'UNICEF' utahusisha shule 3000 za Sekondari na kuwawezesha kupata maudhui ya kujifunza bila gharama yeyote maktaba zilizopo hapa nchini.
Majaribio ya mradi huo ambayo yamefanyika katika shule za Sekondari za kata zilizopo Zanzibar , Dodoma na Mbeya utawezeaha kuwafikia wanafunzi 5500 .
Aidha Mradi huo wa Smartwasomi umefanya upembuzi yakinifu juu ya Hali ya mtandao wa Internet yenye kasi ya 4G ambapo takribani shule 4,200 zilizopo Tanzania bara na 500 za Zanzibar zitapata huduma ya maktaba mtandao bure bila ya kulipiza gharama yeyote hatua ambayo itakwenda kuongeza kasi ya ufundishaji kwa walimu pamoja na kukuza uelewa kwa wanafunzi.
Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Airtel Tanzania Dinesh Balinh ameeleza kuwa "Dhamira yetu kupitia mradi huo wa Smartwasomi ni kuweka shule 3000 kidigitali kwa muda wa miaka mitano ambapo kwa mwaka huu wa 2024 tutaanza na shule 1000kisha Kila shule ya Sekondari iliyounganishwa itakuwa ukipata GB 1200 kwa mwaka ili kuwawezesha walimu na wanafunzi kwenye kujisomea kwenye maktaba kimtandao"
Akizindua mradi huo katika kilele cha maonyesho ya wiki ya elimu, ujuzi na ubunifu yaliyofanyika kitaifa mkoani Tanga Mei 31 ,2023 Waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amebainisha kuwa uwiano uliopota mashuleni kwa wanafunzi na vitabu katika shule mbalimbali zilizopo hapa nchini haukudhi mahitaji kulingana na viwango vilivyowekwa na Serikali.
Aidha Waziri Majaliwa ameipongeza Airtel kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa mataifa 'UNICEF' kupitia mpango huo ambapo itasaidia juhudi za Serikali katika kuongeza upatikanaji wa elimu kiendana na maendeleo ya Teknolojia yaliyopo kwa sasa,
"Serikali tunaipongeza Kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na UNICEF katika mpango huu kwani utaleta matokeo chanya ya kidumi katika nyanja ya elimu, ushirikiano huu hauongezei tu ubora wa elimu bali pia unahakikish watoto wetu Wana zana zinazohitajika ili kuwawezesha kufaulu katika enzi hizi za maendeleo ya kidigitali" amesema Waziri Majaliwa.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ameishukuru na kuipongeza Kampuni ya Airtel Tanzania kwa kuiunga mkono Serikali kupitia mradi huo ambao unakwenda kuboresha hali ya ufaulu masomo ya kidigital watakayoyapata kwenye maktaba mbalimbali sambamba na kuongeza motisha ya ufundishaji kwa walimu.
"Mpango huu utaweka kiwango kipya katika ubora wa elimu na kuwawezesha vijana wetu kustawi katika ulimwengu wa kidigitali , tunawapongeza kwa kuingia mkono jitihada hii tunatazamiakushuhudia matokeo chanya katika sekta ya elimu hapa nchini"
Post A Comment: