Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM Taifa Joketi Mwegelo amewataka vijana wa kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika chaguzi zijazo.

Akizungumza kwenye ziara ya siku moja akiwa Mkoani Iringa Katibu huyo mbele ya vijana amewataka kuacha kutumika kama mgongo kwa kuwabeba viongozi wengine kwa maslahi yao binafsi.

"Niwatake vijana na hapa mnisikilize kwa umakini sana tunaelekea kwenye uchaguzi tujitokeze kwa wingi kugombea nafasi hizi kwani imezoeleka sisi vijana kuwa mbeleko kwa wengine na kuacha kujipigania wenyewe hasa uchaguzi huu twendeni kwa wingi tugombee na tushirikiane kama vijana"

Aidha katibu huyo amesema kuwa vijana wanapaswa kufahamu kuwa kugombea ni haki yao kikatiba na kupitia jumuiya hiyo wameendelea kuwaandaa vijana kupitia mafunzo mbalimbali wanayopata na nchi hii inajengwa na vijana hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha ana shiriki vyema katika uchaguzi iwe kugombea au kupambania chama kiendelee kusalia madarakani.

Pamoja na hayo Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Vijana UVCCM Taifa amesema kuwa Viongozi wao Kupitia Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Taifa Kawaida Ally Kawaida wako tayari kuwasaidia vijana wenye nia ya dhati ya kugombea nafasi za uongozi na kuendelea kuwaweka vijana pamoja.

"Sisi viongozi wenu kupitia mwenyekiti wetu Comred Kawaida tupo tayari kuhakikisha tunawashika mkono vijana kwa namna yoyote hile wenye kutaka kugombea na tutakikisha hili linafanyika na kufanikiwa kwa sababu lengo letu ni kuona vijana tunaingia kwenye ngazi mbalimbali za maamuzi na nina amini kupitia jukwaa hili kila kijana atachukua maamuzi sahihi kwa maslahi mapana ya taifa letu na chama chetu cha mapinduizi"


Share To:

Post A Comment: