Katika kuadhimisha maadhimisho ya kupinga ukatili kwa Wazee Shirika la umeme Tanzania Tanesco Mkoani humo limetumia maadhimisho hayo kumpa tabasamu Mzee wa miaka 82 ikiwa nijitihada za kutambua na Kitandan mchango wawazee hapa Nchini.
Akizungumza tukio hilo Meneja wa Tanesco Mkoa wa Mara NICKSON Babu Alisema wamemuashia umeme Mzee James Gidion Bure Mkazi kiloleli Wilayani Bunda Mkoani Mara mwenye Umri wa Miaka 82 kupitia umeme tayari lengo ikiwa nikuwathamini Wazee kupitia eneo hilo.
"Huu nimwendelezo wa Zoezi letu hasa kwa wazee ambao hawajiwezi kupitia Umeme Tayari tunawawezeka Kupata Mwanga na hiii nidhamira ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuhakikisha anaagiza makundi yote katika kuyahudumia.
Babu ameipongeza Serikali ya DKT Samia Suluhu Hassan kwanamna ambavyo imeendelea Kutenga fedha kwaajili ya kutoa huduma kwa wananchi nawao kama watendaji wanaendelea kuhakikisha wanafugusa kila eneo katika kuwahudumia wananchi wote.
Naye kwa upande wake Mzee James Gidion ameipongeza Serikali kupitia shirika la umeme Tanzania Tanesco kwani kwa Miaka yote hajawahi kutumia umeme ambapo amesema kwa Miaka ambayo Mungu amempa kuishi Duniani anaendelea kumshuru Rais Samia kwanamna ambavyo amegusa maisha yake huku akiomba huduma hizo pia zitolewee na kwa Wazee wengine ili kuhakikisha Wazee wanapewa kipaumbele kama watu wengine.
"Ninamiaka 82 hii Miaka kwangu nikama imeongezeka kwa furaha niliyonayo kwa serikali yangu sikutegemea namimi nitawasha umeme kwa Muda ambao nitautumia nikiwa hai nafurahi Sana zamani tulikuwa tunatumia vibatari na vizinga tu ilikuwa nichangamoto mno ukilala hujui umelala na kitu gani"Alisema Mzee James Gidion Mkazi wa Bunda.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa mara Kanal Evans Mtambi amelipongeza shirika la umeme na Ugavi Nchini Tanesco kwa kuja na mbinu ya kuwasaidia Wazee kwani Tayari macho yao yameaza kupoteza nuru hivyo kuwakumbuka katika nishati niswala la kupongezwa ambapo amewataka vijana na walezi kuhakikisha wanawajali Wazee katika kuwahudumia nakuhakikisha wanaishi maisha Bora nayenye faraja.
Post A Comment: