Naibu waziri wa habari,mawasiliano na teknolojia ya habari Mhandisi MaryPrisca Mahundi amewataka wanawake wenye malengo ya kujiendeleza kiuchumi kutokuwa wabinafsi katika kupeana ujuzi na maarifa ya mafanikio waliopata na kutembea pamoja bila kuwekeana chuki na husuda kwa mafanikio ya mtu mwingine .
Mhandisi Mahundi amezungumza hayo jijini mbeya wakati akizungumza na umoja wa wanawake wenye malengo katika mkutano mkuu wa kundi hilo ambalo sasa lina mtaji na dhamana ya zaidi ya milioni mia sita walizojiwekea
Naibu waziri wa habari,mawasiliano na teknolojia ya habari Mhandisi Marry Prisca akifungua mkutano huo wenye lengo la kufahamiana na wadau ametoa rai kwa wanawake kuendelea kupendana bila kuwa na choyo ya ujuzi na uwezo walionao katika kuhakikisha kila moja anakuwa kibiashara.
Beno malisa ni mkuu wa wilaya ya Mbeya akitoa salamu mbele ya uimoja huo amewataka wanawake kuungana mkono katika nafasi za uongozi na kusaidiana kibiashara pasipo kuingia katika mikopo umiza.
Mwenyekiti wa umoja wa wanawake waliojiwekea malengo (women with Taget)Doris Luvanda pamoja na mhasisi wa kundi hilo Nasra Haonga wakazungumzia malengo yao.
Post A Comment: