Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Balozi Dkt.Emmanuel Nchimbi amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda kwa kusaidia upatikanaji wa Pikipiki mbili zilizoombwa na wananchi kwenye Mkutano wa Katibu Mkuu huyo uliofanyika Jumapili ya Juni 02, 2024, Makuyuni Mjini Monduli.

Balozi Dkt. Nchimbi ametoa shukrani hizo leo Jumatatu wakati wa kukabidhi pikipiki hizo kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika leo Jumatatu kwenye viwanja vya Kilombero Jijini Arusha ikiwa ni muendelezo wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM mkoani Arusha.

Pikipiki hizo zimekabidhiwa kwa Mama mlemavu aitwaye Josephine Nyabenda pamoja na Kijana Kelvin Daniel ambao wote ni wakazi wa Monduli na walimuomba Katibu Mkuu wa CCM na Mkuu wa mkoa wa Arusha kuweza kuwasaidia pikipiki hizo kutokana na matatizo waliyoyapitia na ugumu wa maisha unaowaandama kwasasa.








Share To:

Post A Comment: