1000096990
Mchumi Mkuu, kutoka Wizara ya Fedha Bi. Salome Kingdom amesema ili kuweza kufikia utekelezaji mzuri wa bajeti ya Serikali wadau katika sekta ya habari wametakiwa kuendelea kushirikiana pamoja na Serikali kutoa elimu kwa wananchi ili wasikwepe kulipa kodi kwani 70% ya mapato ya nchi yanatokana na kodi za ndani huku 30% yakitokana na misaada na mikopo nafuu na mikopo ya kibiashara ya ndani na nje.

Bi. Salome ameyasema hayo leo Mei 14,2024 Mkoani Morogoro wakati akitoa mada juu ya uwasilishaji wa bajeti ya Serikali kwa lugha rahisi kwenye kongamano la kutoa Elimu kwa wamiliki wa mitandao ya kijamii nchini.

“Ushiriki wa wananchi katika kulipa kodi na michango mingine ya serikali ni muhimu kwa sababu inasaidia kuimarisha mapato ya serikali, ambayo ni msingi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo,”amesema.

 Aidha, amebainisha kuwa serikali inategemea mapato yanayokusanywa kutoka kwa wananchi ili kuweza kugharamia miradi muhimu kama vile ujenzi wa miundombinu, huduma za afya, elimu, na maji safi na salama.

"Wananchi wanapaswa kuelewa kuwa kulipa kodi siyo tu wajibu wa kisheria, bali ni mchango wao wa moja kwa moja katika kuleta maendeleo ya taifa. Bila mapato ya kutosha, serikali itashindwa kutekeleza miradi mingi muhimu ambayo inalenga kuboresha maisha ya kila Mtanzania,”ameongeza. 

Sambamba na hayo Bi. Salome amesema uwazi na uwajibikaji wa serikali katika matumizi ya mapato ya kodi utasaidia kuimarisha imani ya wananchi na hivyo kuongeza hamasa yao ya kulipa kodi.

Amesema, "Mitandao ya kijamii ina ushawishi mkubwa katika jamii yetu ya sasa hivyo ni muhimu kutumia ushawishi huo kwa njia chanya kwa kuelimisha na kuhamasisha wananchi kuhusu masuala ya msingi kama haya."
1000096963
1000097079
1000096937
1000096961
1000097047
1000097026
Share To:

Post A Comment: