Mwenyekiti wa Taifa wa ACT-Wazalendo ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, leo Jumamosi Mei 18, 2024 amehudhuria, akiwa Mgeni Rasmi, katika Kikao cha Viongozi wa Kamati za Uongozi za Mikoa, Majimbo, Matawi, pamoja na Ngome zake, kutoka Mkoa wa Kaskazini Unguja, ambao umejumuisha Mikoa ya kichama ya Kaskazini 'A' na Kaskazini 'B' Unguja.

Kikao hicho ambacho ni cha Kwanza kwa Mikoa hiyo, tangu baada ya Uchaguzi Mkuu wa Chama hicho mapema Machi Mwaka  huu; na pia Muendelezo wa Vikao vilivyobeba Maudhui  ya Viongozi Wakuu Kutoa Shukran zao kwa Wanachama wa ACT- Wazalendo; pamoja na kulenga katika Kuimarisha Chama, ambavyo vilianza April 2024 huko kisiwani Pemba,  kimefanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Amali Mkokotoni,  Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Viongozi wa Ngazi mbali mbali wa Chama hicho, wamehudhuria hapo, wakiwemo Makamu Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo Zanzibar, Ndg. Ismail Jussa;  Katibu wa Oganaizesheni na Wanachama, Ndugu Omar Ali Shehe na Makamu Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana Taifa, Ndg. Nassor Marhoun.

Share To:

Post A Comment: