Naibu Waziri wa Madini na Mbunge wa Jimbo la Longido Mkoani Arusha,Dkt Steven Kiruswa amesema kuwa serikali ina fursa nyingi za kujikwamua kiuchumi kwa vijana,wanawake na walemavu hivyo vijana wa Jimbo hilo wanapaswa kujiandaa kabla ya kujitosa katika ajira mbadala ili wawezee kujikwamua kiuchumi.

Waziri Kiruswa alisema hayo Jimboni Longido katika Kongomano la vijana wa wilaya hiyo lililohudhuriwa na vijana zaidi ya 300 wa jimbo hilo ambalo kongamano hilo limeandaliwa na Mbunge huyo kwa ajili ya kuwaanda vijana kujikita katika ajira mbadala zilizopo serikalini na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na Chama Cha Mapinduzi {CCM} Longido.

Alisema kongamano hilo la kwanza Mkoani Arusha na nchi kwa ujumla ambalo wawezeshaji walikuwa wataalamu kutoka Wizara tano za serikali ikiwemo wizara ya Madini ,TAMISEMI ,Mifugo na Uvuvi,Kilimo na Ofisi ya Waziri Mkuu lengo lilikuwa kuwaandaa vijana wa Longido ambao wengi wao ni wa jamii ya kifugaji kutumia fursa zilizopo katika wizara hizo kujikwamua kiuchumi na sio kusubiri ajira serikalini.

Kiruswa alisema serikalini kuna fursa nyingi kwa ajili ya kujikwamua na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amejenga mazingira mazuri ya kuwawezesha vijana,wanawake na walemavu kujikwamua lakini aliwaasa vijana wa Monduli kujianda kwanza  na kujipanga na kuwa na maono ya fursa unayohitaji ili uweze kujikwamua.

Alisema vijana wengi Jimboni Monduli wamekopa fedha katika Halmashauri ya Longido lakini hakujipanga na kujikuta wakitumia fedha hizo kwa njia nyingine ambazo hazikuwa rasmi na kutokana na hali hiyo ameona vijana kupota semina ya namna ya matumizi bora ya fedha kabla ya kwenda kukopa ili fedha hizo zitumike katika kusudia lililokusudiwa.

‘’Vikundi 245 vya vijana,wanawake na walemavu vimepata mafunzo katika kongamano hilo lililowezeshwa na wataalamu kutoka katika wizara hizo nne ili makundi hayo yakikopa fedha zoweze kutumia kama yalivyokusudiwa’’alisema Kiruswa

Naye Mkurugenzi wa Maendelea ya Vijana Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt Mwiga Mbesi kwanza alimsifu Mbunge wa Longido kwa kuandaa kongamano hilo la vijana la kuwanoa ili waweze kuwa na matumizi bora ya fddha kabl aya kukopa na kuwataka wadau wengine katika Halmashauri kuiga mfano huo.

Alisema Ofisi ya Waziri Mkuu ndio msimamizi mkuu wa sekta zote serikalini na fursaza kujikwamua ziko nyingi vijana wa Longido kwa kushirikiana na Mbunge ni wakati wao wa kujianda kiakili kutumia fursa hizo.

Naye Afisa Utafiti kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Dkt Angelo Mwilawa alisema kuwa vijana katika Jimbo la Longido bado hawajaitumia vema sekta ya mifugo kwani sekta hiyo ina furasa nyingi za kujikwamua kiuchumi.

Mwilawa alisema jimbo la Longido lina vijana 45,000 wakike na kiume na vijana hao wote hanawana ajira rasmi hivyo ni wakati wao wa kujikita katika sekta ya mifugo kwani sekta hiyo bado katika jimbo hilo hajitatumika vema kwa ajili yao.

Mkuu wa Wilaya ya Longido,Marco Ng’umbi amewataka vijana kutumia kongamano hilo kutoa katika utegemezi ili waweze kujiajiri na kujikwamua kiuchumi kwani fursa zilizoko serikali ambazo wataalamu wamezieleza hazijatumika ipasavyo katika wilaya hiyo yenye wakazi wengi wa kifugaji.











Share To:

Post A Comment: