Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mkoani Dar es salaam, Edward Mpogolo, amefungua mashindano ya Umoja wa Shule za Sekondari-UMISSETA Wilaya ya llala

Mashindano hayo yameshirikisha wanafunzi kutoka Majimbo ya Ilala, Segerea na Ukonga kwa ajili kuunda timu ya Wilaya Ilala.

Watakaochaguliwa wataunda timu ya kanda itakayokwenda ngazi ya Mkoa wa Dar es salaam

Mkuu huyo wa Wilaya ya Ilala,  Mpogolo, amefungua mashindano hayo katika viwanja vya Shule ya sekondari Pugu.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya, amesema Michezo ni sera ya chama cha Mapinduzi katika Ilani yake ya Uchaguzi ya mwaka 2020-2025 ambayo ni kujenga afya na mahusiano katika jamii. 

“Leo tunazindua mashindano haya ya Wilaya Ilala nawaomba vijana wangu mkafanye vizuri katika timu ya Kanda muwe na maadili mazuri kambini na nidhamu boramuweze kuleta ushindi katika wilaya yenu kwa kuchukuavikombe vyote “alisema.

Mpogolo amesema ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa kushirikianana Meya wa Halmashauri ya jiji na Mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam watakuwa karibu na Kambi ya Wachezaji wa Ilala mpaka watakapoenda timu ya Taifa.








Share To:

Post A Comment: