Maandiko matakatifu katika kitabu cha Biblia Yakobo 1:27 yanasema Dini safi ni kuwaona yatima,wajane na watu wenye uhitaji wakati Korani takatifu Sura ya 4 aya ya 36 inasema thawabu kwa Waislam ni kutoa sadaka kwa watu walio katika dhiki.

 Hivi ndivyo Taasisi ya Maryprisca Women Empowerment Foundation(MWEF)inayoongozwa Mhandisi Maryprisca Mahundi Naibu Waziri wa Habari Teknolojia ya Mawasiliano na Habari Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya ambaye ndiye Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Mhandisi Maryprisca Mahundi ilivyojitokeza kutoa msaada kwa waathirika wa maporomoko ya mlima Kawetere Kata ya Itezi Jijini Mbeya.

Baraka Mlonga ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Maryprisca Women Empowerment Foundation(MWEF)amesema Mkurugenzi wake Mhandisi Maryprisca Mahundi alitamani kuwepo lakini yupo nje ya nchi hivyo wapokee msaada huo na uwe faraja kwa waathirika.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Itezi Sambwee Shitambala mbali ya kushukuru kupokea msaada huo ameomba wasisisite kurudi tena kwani bado msaada unahitajika zaidi.

Neno la shukurani kwa niaba ya waathirika ilmetolewa na Upendo Mwakasendo ambaye amewashuru wote walioguswa kuwasaidia katika kipindi hiki kigumu wanachopitia kwani wengi wao wamepoteza kila kitu vikiwemo vyakula,mavazi na fedha.

Bado msaada wa kibinadamu unahitajika sana kwa wananchi hao vikiwemo vyakula,nguo na malazi kutokana na wananchi hao baadhi kushindwa kuokoa vitu vyote vilivyokuwemo ndani.

Share To:

Post A Comment: