Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha  Loy Thomas Ole Sabaya amezungumza hayo alipotembelea Shule ya Msingi Losirwa iliyopo kijiji cha Kirtalo kata ya Soitsambu iliyojengwa na Serikali kupitia mradi wa boost, jumla ya shilingi milion 638.2 za kitanzania zimetumika. Shule hiyo inamajengo 18 yakiwemo majengo ya madarasa, jengo la utawala, nyumba ya Walimu inayobeba familia mbili.

Shule hiyo imekamilika na imenza kupokea Wanafunzi mwezi wa januari 2024, na masomo yanaendelea kwa Wanafunzi hao, kamati imeridhishwa na hali nzuri iliyopo shuleni hapo kwani mazingira yanavutia pia ni rafiki kabisa kwa Wanafunzi.

Aidha Mwenyekiti wa CCM Mkoa ametoa rai kwa Wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili waje kuwa wataalamu wazuri watakaolisaidia taifa na wasikimbilie kuolewa au kuoa mara baada ya kumaliza elimu ya msingi, pia amewataka Wazazi kuwapa mahitaji muhimu ya shule watoto ili waweze kusoma bila changamoto ili baadae wae msaada kwao.

“Nataka msome kwa bidii ili mje kuwa Walimu, Madaktari, Maafisa Elimu, ikibidi muwe viongozi wakubwa wa baadae wa nchi hii” amesema Ole Sabaya

Mwenyekiti wa chama ameendelea kusema anawapongeza viongozi wa Wilaya ya Ngongongoro, kuanzia Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji, Afisa Elimu bila kuwasahau Walimu wa Shule ya Losirwa kutoa ushirikiano kwa Wananchi kwani ndio chachu na chanzo cha mafanikio na hiyo ndio njia pekee ya Serikali ya awamu ya sita kuonekana inafanya kazi hususani pale miradi ya maendeleo inapokamilika.

Aidha Mhe. Sabaya amewapongeza wananchi wa Kirtalo kwa ushirikiano waliyonao na kuwataka Wazazi kuhakikisha watoto wanafika shuleni

“Niwapongeze wananchi wa hapa kwa kujitolea na kufanya kazi nzuri sana hasa kwa kuamua na kujitolea kuajiri Walimu wengine ili waongeze nguvu kazi kwa Walimu waliyoletwa na serikali, ninachowaomba muhakikishe watoto hawa wanafika mapema na tabia ya kuwaozesha watoto wakike hapana waacheni wasome maana ndio watakao tutunza”- aneongezea Mhe. Sabaya

Namshukuru Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa juhudi za dhati anazozifanya katika kuleta maendeleo katika nchi yetu.

Wananchi wa Kirtalo wameishukuru Kamati ya Siasa kwa kufanya ziara hiyo maana inanyoshesha hali ya kuwajali Wananchi na wametoa pongezi kwa Serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kujali.

“Mhe. Mwenyekiti sisi tunakushukuru kwa kuja wewe pamoja na Kamati sisi kama Wananchi tumefurahi na tunakuomba uendelee kuja zaidi pia tunamshukuru Mhe. Rais kwa kuendelea kutujali”-Nikson

Kamati ya Siasa Mkoa wa Arusha ikiongozwa na Mhe. Sabaya imefanya ziara mahsusi ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa Wilaya ya Ngorongoro na kuhakikisha fedha zinazoletolewa na Serikali zinatumika ipasavyo. ziara ya siku tatu wilayani Ngorongoro inayotarajia kumalizika tarehe 6 Machi, 2023

Share To:

Post A Comment: