Na Dickson Mnzava 

Makamu wa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango amezitaka mamlaka za uhifadhi wa misitu Nchini kujipanua na kutoa elimu zaidi kwa wananchi namna ya kupanda miti ambayo inaendana na utunzaji wa vyanzo vya maji.


Makamu wa Rais DKT. Mpango ametoa agizo hilo wilayani Same Mkoani Kilimanjaro katika maadhimisho ya siku misitu duniani pamoja na upandaji miti kitaifa maadhimisho ambayo yanafanyika kitaifa wilayani Same Mkoani Kilimanjaro.


Amesema mwanzoni Nchi ya Tanzania ilikuwa na vyanzo vingi sana vya maji lakini vimekuwa vikipungua Kutokana na uharibifu wa mazingira pamoja na uoteshaji miti ambayo ni adui kwenye vyanzo vya maji.

"Nakumbuka sana mwanzoni Nchi hii ilikuwa na vyanzo vingi sana vya maji lakini vimekuwa vikipungua kila leo Kutokana na uharibifu wa mazingira pamoja na uoteshaji miti isiyorafiki kwenye vyanzo vya maji mfano wa miti ambayo ni adui mkubwa sana wa vyanzo vya maji ni mti aina ya mkaratusi mti huu umekuwa ukiotesha kwenye vyanzo vya maji maeneo mengi Nchini na wananchi pasipo kujua athari yake hivyo ifike mahali sasa nyie wataalam mshuke vijijini kuwaelimisha wananchi aina za za miti ambayo ni rafiki na vyanzo vya maji ili kuendelea kutunza vyanzo hivyo kwa manufaa ya kizazi cha sasa na hata kizazi cha baadae "

"Alisema DKT.Mpango".


Katika hatua nyingine makamu wa Rais DKT.Mpango amewataka wananchi kote Nchini kutumia nishati m'badala ya gesi katika matumizi ya nyumbani kwenye kupikia na kupunguza matumizi ya kuni na mkaa ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakichochea ukataji wa miti kiholela kwenye maeneo mbalimbali ya wananchi.



Waziri wa maliasili na utalii Nchini Angellah Kairuki kwenye maadhimisho hayo amesema miongoni mwa wilayani zinazokabiliwa na changamoto kubwa ya ukame Nchini ni pamoja na Wilaya ya Same kwani wananchi wake wamekuwa wakifanya shughuli ambazo zinakinzana na mazingira.


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu amesema kwenye maadhimisho hayo kama Mkoa wamekwisha otesha zaidi ya miti milioni nane kwenye maeneo mbalimbali ndani ya Mkoa huo.



 

Share To:

ASHRACK

Post A Comment: