Katibu tawala wa wilaya ya Nachingwea Haji Mubaruk Balozi akiongea wakati wa uzinduzi wa wiki ya sheria wilaya ya Nachingwea 
Katibu tawala wa wilaya ya Nachingwea Haji Mubaruk Balozi akisalimiana na wachezaji wakati wa uzinduzi wa wiki ya sheria wilaya ya Nachingwea 


Na Fredy Mgunda, Nachingwea.

 

Katibu tawala wa wilaya ya Nachingwea Haji Mubaruk Balozi ameitaka sekta ya mahakama kusimamia haki kwa uwazi ili haki hiyo ionekane imetendeka kuwezesha kuchochea ustawi katika jamii na kuleta maendeleo ya nchi.

 


Balozi amesema hayo akizindua wiki ya sheria ikiwa ni ishara ya kuanza rasmi kwa kushughuli za mahakama uzinduzi uliofanyika kwenye viwanja vya Saba Saba Nachingwea 

 

 Alisema kuwa maendeleo kwa kiasi kikubwa yanategemea kuwepo kwa utendaji haki na mahakama ndiyo chombo kilichopewa mamlaka na madaraka ya kusimamia jambo hilo.

 


Balozi alisema kuwa haki huinua Taifa na kwamba bila haki hakuna maendeleo katika taifa lolote,unapiga hatua za maendeleo kwa haraka na kwa sasa serikali imetoa fedha nyingi kutekeleza miradi wilaya ya Nachingwea hivyo ni lazima suala la utendaji haki liwe linaonekana wazi katika utendaji wa idara ya mahakama.


Akizungumza wakati wa uzinduzi wa wiki ya sheria wilaya ya Nachingwea yenye kauli mbiu inayosema “Umuhimu wa dhana ya haki kwa ustawi wa Taifa:Nafasi ya mahakama na wadau katika kuboresha mfumo jumuishi wa haki jinai” Sikitu Mwalusamba Hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya ya Nachingwea alisema kuwa wamekuwa wanatoa elimu ya sheria kila wakati hivyo amewaomba wananchi kujitokeza kupata elimu hiyo kila inapotokea.


Mwalusamba alisema kuwa lengo la kutoa elimu ya sheria katika wilaya ya Nachingwea ni kuwasaidia wananchi kuzijua haki zao za msingi ili wasidhurumie haki pale inapotokea Kuna mgogoro wa kisheria.


Alisema katika wiki hii ya sheria wamejipanga kwenda kutoa elimu ya sheria katika soko kuu la wilaya ya Nachingwea,shule ya wasichana wa Nachingwea na Kilimarondo lakini kutakuwa na shughuli mbalimbali ambazo zitafanyika katika wiki hii ya sheria wilaya ya Nachingwea.

 

Share To:

Post A Comment: