Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha imeipongeza Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa kusimamia ipasavyo miradi wanayoisimamia ikiwemo mradi wa jengo jumuishi la wagonjwa wa nje (OPD Complex) katika hospitali ya wilaya iliyopo Njiro Jijini Arusha.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa Thomas Loy Sabaya pamoja na Mwenyekiti wa Umoja wa Jumuiya ya Wanawake Mkoa wa Arusha (UWT) Florah Zelothe kwaniaba ya wajumbe wa kamati hiyo ya CCM Mkoa wa Arusha.
 
Jengo hilo la wagonjwa ambalo linagharimu shilingi Bilioni tatu milioni mia tisa sitini na tano (3.965 Bil.) hadi kukamilika kwake ambapo lina uwezo wa kuchukua wagonjwa/wateja 1000 kwa wakati mmoja. Jengo hilo pia litakuwa na uwezo wa kutua Helkopta ya wagonjwa wa dharura kutoka nje ya Jiji la Arusha hasa raia kwa kigeni.
 
Sabaya alisema ujenzu wa  jengo hilo ni ubunifu mkubwa uliyofanywa na Halmashauri ya Jiji la Arusha katika kukuza sekta ya Afya hapa nchini na kuunga juhudi za Rais Dkt, Samia Suluhu Hasan za kukuza na kuboresha sekta ya Afya nchi nzima
 
”Uwepe wa jengo hili litakapokamilika litawezesha kusogeza huduma za afya kwa wananchi wa halmashauri ya Jiji letu sanjari na kupunguza rufaa nyingi na msongamano wa wateja kwa hospitali ya Mkoa wetu”. alisema Sabaya.
 
“Tunawapongeza kwa kusimama vema miradi ya Jiji sanjari na kuvunja mikataba wa awali na mkandarasi kuomba ongezeko la gharama ya mkataba kwa asilimia 19 na kusababisha kukamilika kwa wakati kwa hosptali yetu”.alisema Zelothe
 
Pia Sabaya alisisitiza ujenzi huo kukamilika haraka ili wananch waanze kupata huduma kutokana na ujenzi huo upo nje ya muda kutokana na changamoto za awali za mkandarasi wa kampuni ya B.H Ladwa kuomba ongezeko la juu zaidi lakini mara alipofika Mkurugenzi wa Jiji la Arusha,Injinia Hamsini jengo hilo limeendelea kujengwa kwakutumia mfumo wa Force Akaunti ambayo inawatumia wazabuni wenye bei nafuu ya gharama ya vifaa vya ujenzi.
 
Akisoma taarifa za mradi huo  Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha Dk, Maduhu Nindwa alisema mradi huo wa ghorofa tatu utatumia kiasi cha sh,bilioni 12 lakini gharama za mradi huo awamu ya kwanza zinakadariwa kuwa ni sh, bilioni, 3 huku gharama nyingine zikitumika kwaajili ya kumlipa mkandarasi Sansutwa Simtali Limited na kueleza ujenzi huo umefika asilimia 70 ya ujenzi huo.
 
Pia Dkt, Nindwa alisema kuwa changamoto kubwa katika mradi huo ni kupanda kwa gharama ya vifaa vya ujenzi na kulazimika kuongezeka kwa gharama za mradi sanjari na manunuzi ya vifaa vya ujenzi kupitia mfumo wa manunuzi wa NeST kuchukua muda mredu kupata mahitaji ya vifaa vya ujenzi.
 
Jengo hilo litakapokamilika litakuwa na maeneo ya Idara ya dharura,ushauri na usafishaji damu,Idara ya mionzi ikiwemo MRI Ultrasound,CT Scan na huduma za uchunguzi wa mwili mzima,Idara ya watoto,maabara,mionzi tiba na huduma nyinginezo muhimu.
Kamati ya siasa ya CCM Mkoa wa Arusha inaendelea kukagua utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya zote za Mkoa huo.
Share To:

Post A Comment: