Wataalamu wa mionzi (Radiographer) wanaotoa huduma ya uchunguzi wa matibabu kwa kutumia mionzi kutoka katika hospital zaidi ya 80 nchi nzima wemekutana hii leo jijini Arusha kwaajili ya kupatiwa mafunzo ya matumizi sahihi ya vyanzo vya mionzi ikiwa na lengo la kuboresha usalama wa Afya za wagonjwa.

Akifungua mafunzo hayo Mkuu wa Idara ya huduma za ufundi na Kinga ya mionzi,Yesaya Sungita amesemakuwa mafunzo haya nikuhakikisha kwamba kuna usalama mahali wanapofanyia kazi kwa mtuamiaji wa mionzi na mtaalam"Usalama tunaangalia wewe mwenyewe na kujilinda na mionzi ni kitu cha kwanza kwasababu wewe n binadamu unapaswa kujilinda ilikuepukana na madhara ya mionzi "alisema

Mafunzo haya ambayo hutolewa kila mwaka kwa makundi yote ambayo hutumia vifaa vya mionzi, ikiwamo wataalamu wa afya yanatajwa kuleta chachu ya kupunguza madhara yatokananyo na mionzi ikiwamo kulinda mionzi isiweze kudhuru wagonjwa.

Pia amesema kuwa kwa wale wanaohudumia wagonjwa wawe na umakini katika kazi yao na vifaa wanavyotumia maana mgonjwa anategemea kupata unafuu kutoka kwao na kupata ahueni kutokana na huduma anayoipata kupitia wataalamu hao.

Hata hivyo amesema kuwa mafunzo haya yatawaimarisha na kuwaongezea  juhudi zaidi na mbinu  yakuhakikisha kwamba yule mgonjwa na anayemleta wanarudi wakiwa salama.

Vilevile Mteknolojia Nassoro Ally kutoka hospital ya Ampolla iliyopo Zanzibar amesemakuwa mafunzo yanawafundisha kuwa ni namna gani wataweza kutumia mionzi kwa matumizi yaliyokuwa salama zaidi na pia itawasaidia kujitambua na kuongeza umakini katika kazi kutokana na kutambua matumizi ya dozi ya mionzi na madhara yake kutokuwa makubwa.

"Kuna watu ambao wanatumika tuu baadhi ya sehemu kufanya X-ray wakijua ni kubonyeza lakini hawajui kuwa ile mionzi inayotoka inapomfikia mgonjwa kwa kiasi kinachopitiliza inakuwa na madhara zaidi"alisema daktari Nassoro

Kupitia mfumo huu wa  mafunzo wataenda kujua kituo gani kina leseni na kipi hakina na kumjua "Radiographer "sahihi jambo ambalo litaenda kutatua tatizo kwa wale wataalamu ambao bado hawajajua kiasi cha mionzi na matumizi yake katika mwili ya Binadamu. 

Naye Mteknolojia wa mionzi kutoka hospital ya Moyo ya Jakaya Kikwete Kassimu Jumanne amesema mafunzo haya yatawaongezea ujuzi zaidi na kuwakumbusha hata yale ambayo walijifunza wakiwa shuleni na hawakupata muda wakuyafanyia kazi kupita mafunzo haya watakumbuka na kuyatelekeza vyema katika upatikani wa huduma hiyo kwa wagonjwa


Share To:

Post A Comment: