.....................................
Na Dotto Mwaibale, Singida
TAASISI ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) imezindua awamu ya pili ya Mpango wa Elimu Changamani kwa vijana walio nje ya shule (MECHAV/IPOSA) kwa ufadhili wa Sh. Milioni 6 dola za Kimarekani zilizotolewa na Serikali ya Korea Kusini kupitia Shirika la Koica ambao umezinduliwa Novemba 18, 2023 mkoani Singida ukilenga kuwakwamuwa vijana kielimu na kiuchumi.
Katibu Tawala Mkoa Singida, Dkt. Fatma Mganga akizindua mpango huo mkoani hapa kwa niaba ya mikoa sita ambayo mpango huo utatekelezwa kwa awamu ya pili ametoa ushauri kwa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kuangalia upya sera na sheria inayoelekeza mwanafunzi asiye hudhuria shuleni
kwa muda wa siku 90 kufutwa baada ya kupoteza sifa za kuwa mwanafunzi.
Dkt. Mganga ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo alisema sheria hiyo imekuwa ikiongeza idadi kubwa ya vijana walio nje ya Mfumo Rasmi wa Elimu Changamani (IPOSA).
Alisema kuwepo kwa sheria hiyo kunaweza kuwafanya baadhi ya wazazi na
walezi wasiopenda watoto wao kusoma kuwazuia wasiiende shuleni kwa muda huo kwa
kuwa watakuwa wamejiondoa wenyewe hivyo kusababisha idadi kubwa ya watoto
kuwepo mitaani bila ya kujua kusoma, kuandika na kuhesbabu.
Dkt. Mganga aliwataka maafisa elimu, watendaji wa Kata, maafisa Tarafa na
viongozi wengine kufanya jitihada za makusudi katika maeneo yao ili kuwabaini
watoto ambao hawaendi shuleni ili wajue kwanini wapo nyumbani na kuwarudisha
shuleni.
Alisema Mkoa wa Singida wanafunzi wanaomaliza darasa la saba ufaulu wao
haupo vizuri upo asilimia 76 jambo ambalo
si zuri ukilinganisha na mikoa mingine.
Alisema mpango huo wa IPOSA ni fursa kwa vijana walio nje ya shule kwa kuwa unalenga kupunguza idadi ya vijana walioko mitaani kwa kuwajengea stadi za
maisha, stadi za ujasiriamali, stadi za Kusoma, Kuhesabu na Kuandika na stadi
za Ufundi wa Awali na hatimaye kupata fursa za kujiajiri au kuajiriwa.
"Mpango huu umezingatia dhima ya Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia ya kutoa Elimu bora kwa wote, Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka
2014, toleo la 2023 inayolenga pia kutoa mafunzo ya amali kwa vijana na Mpango
wa Maendeleo ya Elimu," alisema Dkt.Mganga.
Alisema mpango huo unaendeleza utekelezaji wa azma ya Serikali
kutoa Elimu kwa Watoto na Vijana kupitia mfumo rasmi na usio rasmi.
Aidha, Dkt. Mganga alisema amefarijika kufahamu kuwa baada ya utekelezaji
wa wa mpango huo katika mikoa 10
sasa wanaelekea kwenye upanuzi wa huo kwenye mikoa sita zaidi
na kufikia mikoa 16 ya Tanzania bara na kuitaja mikoa hiyo sita kuwa ni
Pwani,Tanga, Manyara, Simiyu, Singida na Shinyanga kwa ufadhili wa KOICA.
Alisema mikoa hiyo ilipatikana kwa kuzingatia uwepo wa vijana wengi kati ya
umri wa miaka 14 na zaidi waliopo nje ya shule, utayari wa mikoa katika
utekelezaji wa mpango huo , uwepo wa walimu wa ufundi na uwepo wa miundombinu
pamoja na PPTCs.
Alisema mpango huo ulioanza kutekelezwa kwa ufadhili wa KOICA zitajengwa karakana mpya 30
kwa ajili ya mafunzo, ununuzi wa
vifaavipya vya kufundishia ufundi na kufadhili mafunzo ya muda mfupi ya
walimu 240 na mafunzo ya diploma ya elimu ya watu wazima na teknolojia kwa
walimu 120.
Aliongeza kuwa vilevile vitajengwa vituo 3 vikubwa vya mafunzo ya walimu
watakaosoma diploma ya elimu ya watu wazima na teknolojia katika mikoa ya
Tanga, Manyara na Shinyanga.
Alisema kwa hatua hiyo inadhihirisha jitihada walizozionesha na kuwapa
imani wafadhili na kuendelea na awamu ya pili, ambapo pamoja na mambo mengine
walifanikiwa kudahili vijana 12,000 (Me 5,406, Ke 6,594) kwa programu ya muda
mrefu na 30,183 kwa programu ya muda mfupi katika kipindi cha miaka mitatu kwa
Mikoa kumi ya Kigoma, Tabora, Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, Dodoma na Dar es
salaam kwa ufadhili ya UNICEF na Mkoa wa Shinyanga kwa ufadhili wa Care
International na Mkoa wa Rukwa kwa ufadhili wa Plan Internatioanal na kuwa kwa awamu hii ya pili wamelenga
kudahili vijana 52,000 mpaka ifikapo mwaka 2026.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Kamishna wa Elimu Wizara ya Elimu Sayansi na
Teknolojia, Oscar Msalila alisema Mpango wa IPOSA ni matokeo ya juhudi za
pamoja kati ya wizara hiyo, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI), Taasisi ya Elimu ya Watu wazima na wadau wa maendeleo UNICEF.
Alisema kupitia mpango wa IPOSA vijana wenye umri kuanzia miaka 14
wameweza kujengewa stadi za ujasiriamali na stadi za ufundi wa awali ili waweze
kujikomboa kiuchumi na kuchangia uchumi wa Taifa.
Alisema katika utekelezaji wa mpango huo wa IPOSA chini ya UNICEF, Care International na Plan
International vijana waliofuzu mafunzo yao wameweza kuunda vikundi vya
kijasiriamali ambavyo vimewawezesha kufanya biashara na kujipatia kipato.
Msalila alivitambulisha vikundi vichache vya IPOSA kutoka Mbeya na Kigoma
ambayo vimeweza kuanzisha bidhaa za taulo za kike ambazo zinaweza kutumika
zaidi ya mara moja pamoja na bidhaa za samani mbalimbali.
Alisema ubunifu wa bidhaa hizo ni muhimu kwa Taifa la Tanzania hasa kwa
watu wa kipato cha chini, madhalani wale ambao si rahisi kumudu gharama za
kununua taulo za kike zilizozoeleka ambazo bei zake kwa kiasi fulani ni kubwa
kidogo.
Alisema zaidi ya kiwanda hicho cha taulo za kike mpango huo umeweza kuzalisha vijana wabobezi katika fani ya umeme na wameweza kutengeneza
mifumo ya kibunifu ambayo ni suluhisho wa ulinzi nyumbani.
Mkurugenzi Mkazi kutoka Taasisi ya Koica, Manshik Shin, alisema Koica ni
chombo muhimu kwa Serikali ya Korea ambacho kinafanya kazi katika miradi
mbalimbali ya maendeleo kwenye nchi 46 duniani ikiwepo Tanzania na kuwa hapa
nchini ilianzishwa rasmi mwaka 1991.
Alisema Koica ilifungua ofisi yake katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
mwaka 2002 na kuwa katika nchi za Afrika Tanzania ni nchi ya pili kunufaika na
miradi inayofadhiliwa na shirika hilo ambapo mpaka sasa jumla ya Sh.Bililioni
22 zimekuwa zikitolewa kufadhili miradi mbalimbali kila mwaka.
Shin alisema Koica imekuwa ikiisadia Tanzania Bara na Visiwani kwenye eneo
la Elimu, Afya, Maendeleo ya Vijijini, Eneo la Jinsia, TEHAMA na masuala
mbalimbali ya mtambuka.
Alisema katika sekta ya elimu Koica imekuwa ikifadhili shughuli za programu
za ufundi, sayansi, uhandisi na hesabu ili kukuza uwezo wa vijana na waweze
kujiajiri.
Afisa Elimu Mkoa wa Singida, Dkt.Elpidius Baganda alisema mpango huo kwa Mkoa wa Singida umefika wakati muafaka kwani kuna vijana wenye umri kati ya miaka 14 hadi 19 zaidi ya 15,000 wenye sifa za kujiunga kwenye mpango huo, kunavija ambao hawakubahatika kwenda shule 672 na walioacha shule 1064, wanafunzi waliomaliza darasa la saba lakini hawakupa fursa ya kuendelea na masomo ni 12, 013, waliomaliza kwa kupitia MEMKWA ni 1260 na walioacha shule kwa changamoto mbalimbali zikiwepo mimba ni 398.Katibu Tawala Mkoa Singida, Dkt. Fatma Mganga, ambaye alikuwa mgeni rasmi akihutubia kwenye uzinduzi wa mpango huo.Mkurugenzi Mkazi kutoka Taasisi ya Koica, Manshik Shin, akizungumzia jinsi shirika hilo linavyofadhili miradi mbalimbali hapa nchini.Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Profesa Michael Ng;umbi, akizungumza kwenye uzinduzi huo.Kwa upande wake Mwakilishi wa Kamishna wa Elimu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Oscar Msalila akizungumza kuhusu mradi huo.Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Profesa Sotco Komba, akizungumzia taasisi hiyo jinsi inavyoshiriki katika mpango huo.Mkurugenzi Idara ta Elimu Mbadala na Watu Wazima Zanzibar, Mashavu Ahamad Faga, akizungumza kwenye uzinduzi huo.Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ernest Hinju akizungumza kwenye uzinduzi huo.Afisa Elimu Watu Wazima na Elimu nje ya Mfumo Rasmi Wilaya ya Kasulu Mkoa wa Kigoma, Felician Ferdnand (kushoto) akiwa na Mratibu wa Kituo cha Ufundi (TRC) cha Mbalizi Mkoa wa Mbeya Mhandisi Lwitiko Mwakatumbula ambapo walipata fursa ya kuelezea mafanikio ya mpango huo wa IPOSA katika mikoa yao kwenye uzinduzi huo..
Post A Comment: