NA FARIDA MANGUBE MOROGORO.


Katika kipindi cha miaka Miwili ya Uongozi Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Mhe. Samia Suluhu Hassani takbribani shilingi Bilioni 61 .45 zimetengwa kwa Mkoa wa Morogoro Pekee kwajili ya Utekelezaji wa miradi ya uboreshaji na ujenzi wa Barabara Vijijini.


Akitoa Taarifa kwa Waandishi wa Habari Meneja wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini TARURA Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Ndyamkama kwenye Mkutano wa Kampeni ya TUMEWASIKIA TUMEWAFIKIA inayoendeshwa na Ofisi ya Habari Maelezo, amesema lengo la Serikali ni kufungua  mawasiliano ya barabara katika maeneo ambayo hayafikiki.


Amesema katika kipindi hicho Takribani Kilometa 190 zimefunguliwa katika maeneo mbalimbali vijijini kwa kulenga maeneo yenye kipaumbele ikiwemo maeneo ya Shule, Hospitali, vituo vya Afya, Soko, maeneo ya shughuli za utaii, kuabudia pamoja na  Kilimo hasa mazao ya Mpunga, Miwa, Kokoa,Mahindi, Ndizi na Mkonge.


Amesema barabara za Changalawe zimeongezaeka kutoka kilometa 987 hadi 1454.75, kiwango cha Rami 87.65 hadi  96.15, barabara za zege ambazo zinadumu kwa zaidi ya mika 70 nazo zimeongezeka kutoka 0 hadi 5.2 huku mpango ikiwa ni kungeza ujenzi wa barabara za zege kwenye maeneo yenye muinuko.


Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima amesema mkakati wa Mkoa kwa sasa ni kujikita katika kufanya mapinduzi ya kilimo Biashara kwenye zao la Mpunga kutoka tani laki 9 za sasa hadi tani 150, ambalo wakazi wengi wa Mkoa huo wamekuwa wakilima kilimo cha mazoea.


Aidha amesema kupitia ujenzi wa miundombinu ya Barabara vijijini utaongeza tija ya bei ya mazao ya wakulima shambani kwani inarahisha usafirishaji wa mazao kutoka shambani kufikia soko la ndani na nje ya nchi.


Naye Mkurugenzi wa Habari maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikari Mobhare Matinyi amesema Serikali ya awamu ya sita imejipambanua katika kuwasikiliza na kuwafikia wananchi hasa katika kutatua changamoto zao moja kwa moja na kuwawekea mazingira rafiki ya kuinua kipato chao.




MWISHO.

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: