AFISA Tarafa ya Ilongero Wilaya ya Singida, Yahaya Njiku amewahimiza
wajasiriamali katika tarafa hiyo kuongeza thamani ya bidhaa wazazozizalisha ili
ziuzwe kwa bei ya juu jambo litakalo saidia kuinuka kiuchumi.
Njiku ambaye alikuwa mgeni alitoa ombi hilo hivi karibuni wakati akifungua
mafunzo ya ujasiriamali kwa wananchi wa
tarafa hiyo ambayo yaliandaliwa na Shirika lisilo lakiserikali Star
Entrepreneur General lenye makao yake makuu mkoani Singida.
Alisema mafunzo hayo ni ya muhimu kwa wananchi wa tarafa hiyo kwani
yamelenga kuwainua wananchi kiuchumi kuanzia ngazi ya familia hadi taifa.
“Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Saluhu Hassani imejielekeza
kuwawezesha wajasirimali na wafanya biashara wadogo ili kukuza mnyororo wa
thamani wa bidhaa wanazozalisha hivyo ni vizuri mkatumia mazingira na rasilimali
zinazowazunguka kwa kuzigeuza kuwa fursa katika uwekezaji,” alisema Njiku.
Njiku alipongeza shirika hilo kwa kuunga mkono jitihada za Serikali kwa
kutoa mafunzo hayo kwa wajasiriamali hao na akaomba mashirika mengine
yaliyoyopo katika wilaya hiyo kuiga mafano wa shirika hilo.
Alisema kupitia mafunzo hayo wananchi wanajiajiri kupitia utengenezaji wa
bidhaa zao ambazo wanaziuza ndani ya Mkoa wa Singida na mikoa jirani.
Naye Mkurugenzi wa Shirika la Star Entrepreneur General Danford Kassaga alisema
mafunzo hayo yatawawezesha wafanyabiashara na wajasiriamali hao kujifunza mbinu
za kibiashara na kujua namna ya kukuza thamani ya bidhaa zao.
Washiriki wa mafunzo hayo walinufaika kwa kujifunza utengenezaji wa vitu
mbalimbali kama sabuni, uokaji wa keki kwa ajili ya sherehe, upikaji wa tambi
za mayai, unga wa lishe, ufugaji wa
kuku,utengenezaji wa batiki pamoja na usimamizi wa biashara na masoko.
Ufunguzi wa mafunzo hayo ulihudhuriwa na Mtendaji wa Kata ya Ilongero, Mohammed Mduma ambae alisisitiza kuyatumia kama chachu ya kubadilisha maisha ya mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla.
Mkurugenzi wa Shirika la Star Entrepreneur General, Danford Kassaga, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.
Afisa Tarafa ya Ilongero Wilaya ya Singida, Yahaya Njiku, akisisitiza jambo wakati akifungua mafunzo hayo.
Post A Comment: