Na Imma Msumba ; Karatu

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe, John V. K. Mongella ameuagiza uongozi wa wilaya Karatu kupitia Mkurugenzi halmashauri hiyo kuhakikisha wanakamilisha mradi wa ujenzi wa Bwalo la chakula liliojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 50 fedha kutoka serikali kuu tangu mwaka 2017.

Rc Mongella amemuagiza Mkurugenzi huyo, kutoa fedha za mapato ya ndani ,kukamilisha bwalo hilo la chakula lilojengwa kwa ajili ya wanafunzi wenye Mahitaji Maalum, mradi ambao umekaa kwa muda mrefu sasa bila kukamilia huku watoto wakihitaji kuhudumiwa kupitia bwalo hilo.

"Ninakuagiza DC na mkurugenzi kutoa fedha kukamilisha jengo hilo na terehe 01.12.2023 nitakuja kufungua, serikali ilishatoa fedha wekeni kipaumbele kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum, Serikali ya awamu ya sita chini ya Mama yetu mama Samia  anawajali watoto wenye mahitaji maalum, kamilisheni mradi huu kwa haraka" Amesistiza Rc Mongella

Hata hivyo ameutaka uongozi wa halmashauri kuhakikisha wanakamilisha miradi yote kwa wakati na viwango vya ubora vinavyoendana na thamani ya fedha, miradi ambayo inayoletewa fedha na Serikali kuu na kukemea tabia ya kutokukamilisha miradi huku fedha zikiwa zimekwisha, amesisistiza kuwa kila fedha za mradi zinakuja zikiwa na maelekezo ya kukamilisha mradi husika.

Awali amesisitiza kuweka vitanda kwenye Bweni la shule hilo ambalo tayari miundombinu yake imekamilika ili siku ya uzinduzi majengo yote yaanze kutumika na wanafunzi hao wenye mahitaji Maalum.Share To:

Post A Comment: