OR-TAMISEMI, NJOMBE

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Dkt.Festo Dugange amesema ndani ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan zaidi ya Sh. Bilioni 8 zimepelekwa katika Mkoa wa Njombe kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba.

Mhe. Dugange ameyasema hayo akiwa katika ziara ya Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango mkoani Njombe alipokuwa akizungumza wafanyakazi wa kiwanda cha mbao cha TAN WAT kilichopo wilayani Njombe.

"Mhe Makamu wa Rais kipekee sana nimshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo ndani ya miaka miwili amefanikiwa kuboresha sekta ya afya katika Mkoa huu wa Njombe. Kiasi cha Sh Bilioni 8 kimeletwa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba na dawa.

" Miaka miwili ya Rais Dkt Samia amejenga Hospitali za Wilaya katika Wilaya ya Wanging'ombe, Njombe Vijijini, Mji wa Makambako huku akipeleka Sh Milioni 900 kwa Wilaya ya Ludewa na Makete kila moja kwa ajili ya ukarabati wa Hospitali," amesema Dkt. Dugange.

Amesema Mkoa wa Njombe ulikuwa una upungufu wa vituo vya afya lakini ndani ya miaka miwili vimejengwa vituo vya afya 17 pamoja na Zahanati 34 ndani ya Mkoa huo.Share To:

Post A Comment: