Mwenyekiti wa cha RUNALI Odasi  Mpunga akiongea wakati wa zoezi la Mnada wa korosho unaondeshwa na chama cha RUNALI Kwa mara ya kwanza Kwa msimu mpya wa korosho na Bei ya juu kufikia shilingi 2030
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akifuatilia Kwa karibu Mnada wa kwanza wa zao la korosho unaondeshwa na chama cha RUNALI


Na Fredy Mgunda, Nachingwea.

MNADA wa kwanza wa zao la korosho wa chama RUNALI umefanyika katika wilaya ya Nachingwea kwa kilo moja ya korosho kuuzwa Kwa kiasi cha shilingi 2032 ikiwa ndio Bei ya juu zaidi huku Bei ya chini ikiwa shilingi 1965.

Akizungumza wakati wa Mnada huo mwenyekiti wa cha RUNALI Odasi  Mpunga alisema kuwa wakulima wote wa zao la korosho wamekubari kuuza Kwa Bei hiyo wakati wa Mnada kwenye maghara yote ya chama cha RUNALI.

Mpunga alisema kuwa korosho ya RUNALI imekuwa korosho bora hadi sasa kutokana na usimamizi mzuri viongozi wa RUNALI wanaofanya wakati wa kupokea korosho hizo gharani.

Alimazia kwa kusema kuwa kwenye Mnada wa kwanza wa korosho uliofanyikia wilaya ya Nachingwea jumla ya kampuni 43 zulijitokeza kununua korosho kwenye chama cha RUNALI.

Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa bodi ya korosho Tanzania Francis Alfred aliwapongeza RUNALI Kwa kupokea korosho zilizokauka vizuri na zenye ubora unaotakiwa sokoni na kuifanya korosho inayotoka RUNALI kuwa namba Moja sokoni.

Alisema kuwa korosho inayotoka RUNALI imepanda sana thamani na kuifanya kuuzwa Kwa gharama kubwa kulinganisha na korosho nyingine za ukanda wa kusini 

Naye mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa korosho zote za msimu huu wa kilimo zitasafirishwa kupitia bandari ya Mtwara ili kuongeza tija ya uwepo wa bandari hiyo Kwa ajili ya kusafisha mazao mbalimbali.

Moyo aliwataka RUNALI kuharakisha malipo Kwa wakulima ili wapate fedha Kwa ajili ya kufanya shughuli za kiuchumi kwenye maeneo wanayoishi.

Pia mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo alizitaka taasisi za kibenk kuendelea kutoa elimu ya kifedha ili wakulima wasiendelee kuibiwa na watu ambao sio waadilifu.
Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: