Na Ashrack Miraji

Kwa kutambua jukumu muhimu linalofanywa na maofisa wa huduma kwa wateja na mawakala wake, Benki ya Tanzania Commercial Bank TCB imezindua Wiki ya Huduma kwa Wateja ambayo inatoa fursa kwa benki hiyo kusherehekea pamoja na wateja wao kwa kuthamini kazi ya maofisa wa huduma kwa wateja katika kuhakikisha viwango bora na furaha ya wateja vinazingatiwa na benki hiyo.

Timu ya Utendaji ya TCB ikiongozwa na Manager wa Kampuni ya Benki Tawi la Wilaya ya Same Mkoani kilimanjaro Mohamed Amri, walikuwa na tukio la kukata keki na kutoa zawadi kwa wateja na wafanyakazi wao kama alama ya kuthamini na kusherehekea Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani iliyoanza Oktoba 2 hadi 7 mwaka huu.

Kaulimbiu yao inasema ‘GROWING STRONGER TOGETHER’ ambayo inajumuisha mambo yote ambayo benki inawakilisha ikiwemo maadili yao ya msingi ikiwemo Ubora, Biashara na Utekelezaji ambayo kwa pamoja yanawafanya kushinda kwa pamoja kama timu.

Alisema wiki hiyo ya huduma kwa wateja ni matokeo ya uthabiti wa TCB katika kuimarisha ushirikishaji wa wafanyakazi na hamasa katika kutoa huduma bora kwa wateja. Katika tukio hilo, maofisa wote wa huduma kwa wateja walipongezwa kwa kazi nzuri na kujituma na kuwajengea imani wateja.

“Lengo letu kuu ni kuonesha falsafa ya kwanza ya C1st kwa mteja kama ‘njia ya maisha’ katika ushirikiano wetu na wateja. Kwa kweli hiki ndiyo kiini chetu na tungetaka kutambulika hivi siku zote, TCB ni taasisi isiyo na shaka katika kutoa huduma bora za kifedha kwa mtazamo wa wateja,”alisema Mohamed Amri

TCB ni benki tanzu ya benki kubwa ambayo inapatikana katika Mikoa yote na wilaya zote hapa Nchin pia ni benki iliyo katika mwelekeo wa kuwa benki pendwa kwa wateja.

Share To:

ASHRACK

Post A Comment: