Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella amezihimiza Hospitali za Rufaa za Mikoa kuwekeza kwenye utoaji wa huduma bora pamoja na uboreshaji wa mifumo ya usimamizi.

Mhe. Mongella ameyasema hayo Sepemba 14, 2023 alipokua akizungumza na waganga wafawidhi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa Mkoani Arusha.

“Ni jambo muhimu kujitathmini kama Sekta kwa kujua umepitia wapi umekutana na nini na malengo uliyojiwekea, hivyo ni muhimu kuwekeza nguvu zenu katika utoaji wa huduma bora na mifumo ya usimamizi”. Amesema Mhe. Mongella

Aidha, Mhe. Mongella amesema kuwa ili kufanikiwa hayo lazima ujiulize kuwa ulifanikiwa kwa kiasi gani katika utoaji wako wa huduma na kama kuna changamoto ni jinsi gani ya kupata mbinu ili kuweza kutatua changamoto hizo.

Pia amesema, Serikali imefanya maboresho makubwa katika Sekta ya Afya katika kila Mkoa ikiwemo Mkoa wa Arusha kwa lengo kuu la kutoa huduma bora kwa wananchi.

"Serikali kupitia Wizara ya Afya imefanya maboresho makubwa kwenye Sekta ya Afya hasa ngazi za Mikoa, Wilaya na Taifa kwa ujumla chini ya usimamizi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan”. Amesema Mhe. Mongella

Hata hvyo, Mhe. Mongella amesema Serikali imeweka fedha nyingi kwenye Sekta ya Afya kwa sababu sayansi ya Maendeleo inasema ukitaka kuendelea, wekeza kwenye rasilimali watu.

“Tukitaka taifa letu la Tanzania liende mbele, lazima tuwekeze kwenye rasilimali watu lakini pia kwenye miundombinu ambapo Serikali imeekeza sana hivyo ni jukumu letu kutoa huduma bora za Afya kwa wananci". Amesisitiza Mhe. Mongella

Vile vile, Mhe. Mongella amezitaka Hospitali hizo za Mikoa kujenga mifumo ya imara ya usimamizi wa Huduma kwa sababu lengo kuu la utoaji wa huduma ni Huduma Bora.

“Eneo hili linahitaji sana huduma bora kwa wateja na mawasiliano mazuri hivyo lazima mawazo yetu yawe chanya kwa kuea wajibu wetu ni kujenga uwezo kwa wafanyakazi wetu ili utoaji wa huduma uwe bora”. Amesema Mhe. Mongella

Mwisho, amezitaka Hospitali hizo kujenge uwezo wa kusimamia mifumo ili kupunguza upotevu wa vifaa tiba, dawa na usimamizi wa mifumo yetu ya bima ili uwezo wa mapato ya Mkoa uwe mzuri.

Share To:

Post A Comment: