Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Thomas Apson (kulia) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru, Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Kemirembe Lwota baada ya kumaliza mbio zake za kukagua miradi katika wilaya hiyo, Septemba 27, 2023.

............................................................

Na Dotto Mwaibale, Itigi

KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023, Abdalla Shaib Kaim ameridhishwa na kupitisha miradi yote ya maendeleo iliyopitiwa na kukaguliwa na Mwenge huo wilayani Itigi mkoani Singida.

Kaim akizungumza na wananchi wa wilaya hiyo Septemba 27, 2023 ikiwa ni siku yake ya tano ya mbio za mwenge alisema miradi yote imetekelezwa vizuri na kuagiza ile yenye mapungufu madogo madogo ifanyiwe marekebisho ndani ya siku tatu.

Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge,  alisema Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imekuwa ikileta fedha nyingi kwenye halmashauri kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali hivyo ni jukumu la watendaji kuhakikisha wanaisimamia ili iwe inajengwa kwa viwango vya ubora ambavyo vinaendana na thamani ya fedha na pia ni njia ya kumuheshimisha.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Kemirembe Lwota  akitoa  taarifa ya miradi iliyotembelewa na kukaguliwa na Mwenge wa Uhuru alisema ni saba na kuitaja baadhi kuwa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya wenye thamani ya Sh.Bilioni 1.9, ujenzi wa barabara ya mijini na vijijini ya mita 700 yenye thamani ya Sh.milioni 499.239, mradi wa maji uliopo Kijiji cha Njirii wenye thamani ya Sh.Milioni 344.9.

Alitaja mradi mwingine kuwa ni ujenzi wa Shule mpya ya Msingi Ukombozi wenye thamani ya Sh.Milioni 496.4, Shule ya Msingi Pentagon wenye thamani ya Sh.Milioni 21.5 mradi wa Vijana (VIKUNDI) wenye thamani ya Sh.Milioni 3.5 na ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi.

Alitaja programu zilizotembelewa na Mwenge huo kuwa ni ya mapambano dhidi ya Malaria ambapo katika kipindi cha Julai 2022 hadi Juni 2023 jumla ya wagonjwa 23,412 walipimwa malaria ambapo wanaume walikuwa 6,337 na wanawake 17,075.

Programu nyingine iliyotembelewa ilikuwa  ni ya mapambano dhidi ya Ukimwi na VVU ambapo wilaya hiyo ina asilimia 4 ya watu waishio na maambukizi ya virusi vya Ukimwi huku idadi ya wanaotumia dawa za ARV ni 3,633 wanaume wakiwa 1,238 na wanawake 2,390.

Programu nyingine ni mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa na kuanzisha klabu katika shule za sekondari, Utoaji wa elimu kuhusu masuala ya lishe na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Lwota alisema Mwenge huo umekimbizwa umbali wa kilometa 77.5.ukifanya shughuli za uwekaji wa jiwe la msingi, uzinduzi na kutembelea miradi hiyo saba na kuwa kauli mbiu ya mbio hizo za Mwenge wa Uhuru 2023 ni Tunza Mazingira, Okoa Vyanzo vya maji kwa Ustawi wa Viumbe Hai na Uchumi.

Mbunge wa Manyoni Magharibi Yahaya Masare alipongeza kazi kubwa inayofanywa na Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo hilo na kuwa hawana cha kumlipa Zaidi ya kumpa kura nyingi katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2025.

Akitoa salamu Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe naye aliungana na viongozi wenzake akiwepo Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Singida kumshukuru Rais Samia kwa kazi kubwa anayoifanya na kutoa fedha nyingi za kutekeleza miradi ambapo aliwaomba wananchi ilipo miradi hiyo kutunza miundombinu yake na aliwaomba kuendelea kumuombea kwa Mungu awe na afya njema.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, Hussein Simba alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwapa ruzuku kutoka katika  bajeti ya nchi ya trioni 7 hadi asilimia 100 ambapo wilaya hiyo inapata Bilioni 8.

Simba alisema mambo hayo zamani yalikuwa hayafanyiki kwani mradi mmoja tu ulikuwa unatekelezwa kwa robo ya bajeti lakini leo hii wanapata asilimia 100.

Kesho Septemba 29, 2023 Mwenge wa Uhuru 2023 unamaliza mbio zake mkoani Singida na utakabidhiwa Mkoa wa Dodoma.

Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Kemirembe Lwota, akimkabidhi risala ya utii Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Abdalla Shaib Kaim.
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Kemirembe Lwota, akimkabidhi cheti Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Abdalla Shaib Kaim katika hafla ya kumkabidhi mwenge huo .
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Thomas Apson akimkabidhi cheti Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Abdalla Shaib Kaim.
Katibu Tawala Wilaya ya Itigi akisoma risala ya utii.
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Kemirembe Lwota, akiteta jambo na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Abdalla Shaib Kaim.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Abdalla Shaib Kaim, akizungumza wakati akiwaaga viongozi wa Wilaya ya Ikungi .
Wakimbiza mwenge wa Wilaya ya Ikungi wakiwa tayari kwa kazi.  
Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi wakiwa  na Mkuu wa wilaya hiyo wakati wa mapokezi hayo.

Vijana wa Skauti wakimvika Skafu Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023 wakati wakimkarisha Wilaya ya Itigi kuanza kukimbiza mwenge huo.

Viongozi wa wilaya ya Itigi wakiwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim wakati wa mapokezi ya mwenge huo..
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, John Mgalula, akiwa ameushika Mwenge wa Uhuru wakati wa mapokezi hayo.
Muonekano wa mradi wa maji Kijiji cha Njirii wilayani humo.
Ukaguzi wa mradi huo wa maji ukifanyika.
Ukaguzi wa tenki la maji la mradi huo ukifanyika.
Wananchi wakishuhudia ukaguzi wa mradi huo wa maji.
Ukaguzi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Itigi ukifanyika.
Waratibu wa programu ya mapambano dhidi ya malaria, Ukimwei na Lishe wakiwa katika ukaguzi wa programu hizo zilizotembelewa na mwenge huyo.
Ukaguzi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Itigi ukiendelea.Muonekano wa baadhi ya majengo ya hospitali hiyo.
Muonekano wa moja ya majengo Hospitali ya Wilaya ya Manyoni ambayo ujenzi wake unaendelea.
Muonekano wa ujenzi wa nyumba ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo
Wakimbiza mwenge wakipitia nyaraka za ujenzi wa nyumba hiyo.
Mbunge wa Manyoni Magharibi akizungumza.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe akizungumza.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya  ya Manyoni Hussein Simba akizungumza.
Ukaguzi wa barabara ya Tarura ukifanyika.
Viongozi wakiwa wamejipanga mistari wakati wakisikiliza ikisomwa risara ya utii.
Wananchi wakiwa kwenye Shamra shamra za mkesha wa Mwenge. 
Shamra shamra zikiendelea Stendi ya zamani ya Wilaya ya Manyoni.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023, Abdalla Shaib Kaim.akipata maelezo alipotembelea banda la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU)  katika Stendi ya zamani ya wilaya hiyo katika shamrashamra za mkesha wa mwenge huo..
Maafisa wa TAKUKURU wakiwa kwenye sherehe za Mwenge kuelekea mkesha.
Wanafunzi wakitoa burudani kwenye sherehe hizo.
Mratibu wa Mbio za Mwenge Wilaya ya Itigi akiwajibika wakati wa sherehe za mwenge
Wananchi wakiwa kwenye sherehe hizo.
Burudani zikitolewa.
Burudani zikitolewa na Wasanii wa Kikundi cha Samia cha kabila la Wasukuma wilayani humo kilipokuwa kikitoa buruda,am
Burudani zikiendelea.
 

Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: