Mbunge wa  Jimbo la Geita vijijini Joseph Kasheku Musukuma (kulia aliyeshika barua) akizungumza na Wavuvi wa Mwaro wa Makatani Kata ya Nkome wilayani Geita ambao wanalalamikia kutozwa faini kinyume na utaratibu.

...........................................................

Na Victor Bariety  Geita 

MBUNGE wa  Jimbo la Geita vijijini Joseph Kasheku Musukuma ameuagiza uongozi wa BMU Mwaro wa Makatani uliopo  Kata ya Nkome wilayani Geita kurejesha fedha zaidi ya Sh.400, 000 walizochukua kwa baadhi ya wavuvi wa mwaro huo ambazo waliwatoza kama faini ya kuvua dagaa wakati wa giza kinyume cha utaratibu.

Mbunge Musukuma ametoa agizo hilo alipofanya ziara ya kushitukiza kwenye mwaro huo kisha kuzungumza na wavuvi wa eneo hilo ambapo bila kumung'unya maneno wavuvi hao walimweleza mbunge wao kuwa uongozi wa BMU kata hiyo wamekuwa wakiwanyanyasa Kwa kuwatoza faini zisizo rafiki pasipo hata kuwapatia risti za malipo hayo.

"Mheshimiwa mbunge  bora umekuja yaani baadhi   ya viongoz wa BMU hapa makatani wanatunyanyasa sana na wamekuwa wakituzuia kuvua dagaa majira ya giza lakini pia wanapotukamata wanatutoza faini ya shilingi elfu hamsini na hatupewi risiti ya malipo hayo" alisema Mussa Juma huku akishangiliwa na wavuvi wenzake na kuongeza mfano juzi tumekamatwa na tumetozwa faini ya Sh.50,000 kila mmoja na hatukupewa risti"

Kufuatia malalamiko hayo Mbunge Musukuma alitaka kupata ufafanuzi kutoka Kwa uongozi Wa kijiji hicho ña kuelezwa KUWA agizo hilo limetoka Kwa uongozi Wa Halmashauri hiyo lengo likiwa ni kuokoa mazalia ya samaki"

Mheshimiwa mbunge siyo kwamba sisi tumejiamulia kuwakamata hawa wavuvi ni agizo kutaka Kwa Mkurugenzi wa Halmashauri na lengo ni kufanya samaki wazaliane"alisema Mtendaji wa Kata ya Nkome John Nzari.

Hata hivyo baada ya maelezo hayo kutoka kwa mtendaji, Musukuma alipitia barua iliyotoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo inayoelekeza utekelezaji wa agizo hilo alihoji iwapo kwenye barua hiyo wameagizwa kuwatoza faini wavuvi hao pasipo kupatiwa risti lakini nakupata majibu yanayojitosheleza.

"Ni kweli hii barua imewaelekeza kukamata wavuvi wanaovua dagaa nyakati za Giza lakini ni wapi ambapo imeelekeza muwatoze faini pasipo kuwapatia risti?" alihoji  Musukuma

kufuatia hali hiyo mwenyekiti wa BNU kata hiyo Ntuzu Emmanuel alijitetea kuwa walikuwa na mpango wa kuwaita wavuvi hao ili wawapatie risti zao uteteziambao pia uligonga mwamba kwa mbunge huyo na kuamuru pesa hiyo irejeshwe haraka Kwa wavuvi hao na iwe mwanzo na mwisho kuwatoza wavuvi hao pesa zao pasipo kuwapatia risti.

"Sasa nisikikizeni naomba pesa uliyochukua Kwa wavuvi muirejeshe Mara moja na iwe mwanzo na mwisho kuwatoza faini pasipo kuwapatia risti, mnasikia nyie wavuvi msikubali kutoa hela bila kupewa risti hata serikali inasisitiza unapofanya malipo ya aina yoyote ile dai risti" alisema mbunge Musukuma huku akipigiwa makofi

Kufuatia Hali hiyo uongozi huo Wa bmu ulimhakikishia Mbunge pesa yote watairejesha na kwamba suala hilo halitajitokeza tena.

Katika hatua nyingine wavuvi hao walimtaka mbunge huyo kuondoka na mtendaji wa kijiji hicho Salum Mussa Kapami kwa madai amekuwa ni mungu mtu.

"Mheshimiwa mbunge uondoke na mtendaji wa kijiji amekuwa amekuwa  Mungu mtu tunaomba uondoke naye" alisema Geradi masaga huku akishangiliwa na wavuvi wenzake

Aidha, akijibu malalamiko hayo Musukuma alimtaka mtendaji huyo kujibu hoja za wavuvi hao na kudai KUWA anasingiziwa

"Ninakuomba ujirekebishe ukiendelea hivyo nitaongea na mkurugenzi akuondoe maana wameshaondoka watendaji wengi sana hapa ambao hawawezi kutatua kero za wananchi" alisema Musukuma.


Ukutano na wavuvi ukiendelea.
Barua kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Geuta ikisomwa na kuoneshwa katika mkutano huo.
 

Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: