Chama Cha mapinduzi CCM Mkoa wa Arusha kimetoa tamko kuhusu ujenzi wa mradi wa standi ya kisasa ya mabasi yaendayo mikoani inayo tarajiwa kujengwa hivi karibuni maeneo ya bondeni city Jijini Arusha.

Seipulan Ramsey katibu wa Siasa na uenezi Mkoa wa Arusha ameyazungumza hayo wakati alipokua akitoa taarifa fupi mbele ya waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali kwa lengo la kuwafikia wananchi wa Mkoa huo.

Akisisitiza kuhusu ujenzi wa stendi hiyo amesema kuwa changamoto iliyokuwa inazuia kuanza kwa ujenzi wa mradi huo imetatuliwa kwa kuliondoa jinamizi lilikua linasumbua kwa miaka mingi.

"Tunatengeneza stendi kubwa na ya kisasa ya mabasi ya mikoani,lile jini au jinamizi lililokuwa linatusumbua tokea enzi za Hayati Rais Magufuli sasa Mama yetu Rais Samia Suluhu Hassan amelimaliza hakuna tena siasa katika eneo la Bondeni City ni mwendo wa kazi katika Mkoa wetu wa Arusha" Alisema

Hata hivyo Saipulani alieleza kuwa wiki iliyopita Jiji la Arusha walitia saini mkataba wa mradi wa uboreshaji wa miundombinu ya Miji Tanzania (TACTIC) ambapo katika mkataba huo walisaini ujenzi wa barabara za lami Engosheraton kilomita 4.8,barabara ya olasiti kilomita 4 pamoja na barabara ya Oljoro itakayoelekea katika eneo inapojengwa stendi ya mabasi.
Share To:

Post A Comment: