Na mwandishi wetu Mbeya

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Juma Homera amezindua mabasi mapya ya kisasa Achimwene safari na kuipongeza   kampuni hiyo kwa kuendelea kufanya uwekezaji huo mkubwa ndani Mkoa na Tanzania kwa nia ya   kumuunga mkono Rais  Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kukuza uchumi wa Nchi.

Mhe.Homera amezindua mabasi hayo leo Agost 12, 2023 akimpongeza  mkurugenzi wa kampuni hiyo Bwana Heneriko Achimwene kwa uzalendo mkubwa huku akisema uzinduzi huo utawapa ajira vijana wa kitanzania. 

Mhe.Homera amesema serikali ya Mkoa wa Mbeya itaendelea kuunga mkono jitihada za kampuni ya Achimwene na kuwataka kuongeza uwekezaji zaidi na zaidi.

Pia amewaomba wananchi mkoani humo  na watanzania kumuunga Mkono muwekezaji huyo ili aendelee kuwekeza  kwamanaana mabasi hayo ni ya kisasa yana Miundombinu ya kisasa na yataepusha ajali za Barabarani kwa kupunguza usumbufu wa abiria kushuka shuka kujipatia huduma za kibinadamu.


Aidha ametoa Rai kwa madereva wote Tanzania kuendesha mabasi kwa kufuata sheria za barabarani kuepusha ajali zisizo za lazima nakwamba sheria zitafuatwa kwa watakao kiuka utaratibu wa nchi.

Nae mkurugenzi wa kampuni ya Achimwene Bwana Heneriko Achimwene ameishukuru sana serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa ushirikiano mkubwa mpaka Vijana kuonekana  kufanya uwekezaji nchini.

Pia Mtendaji Mkuu Bwana Innocent Joseph amewashukuru sana watanzania wote kwa kuendelea kushirikiana na kampuni ya Achimwene na kwamba mabasi hayo niya watanzania zikiwa na safari zake  kutoka Mbeya kwenda dar es salaam na kutoka Dar es salaam kwenda Mbeya kila siku.Katika hafla hiyo ya uzinduzi wa mabasi  mapya Achimwene safari wadau mbalimbali walihudhuria akiwemo msanii wa kuigiza sauti za viongozi Oscar Nyerere kama balozi wa mabasi hayo.

Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: