Na; Elizabeth Paulo, Dodoma


Maafisa ugani watakiwa kwenda vijijini kutoa elimu juu ya ufugaji bora wenye tija kwa ajili ya manufaa ya mtu mmoja mmoja hata Taifa kwa ujumla.


Rai hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa halmashauri ya Bahi na Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa Mhe. Donard Megitii katika ufunguzi wa kongamano la kuku Agost 6, 2023 Katika viwanja vya maonesho ya nanenane Nzuguni Jijini Dodoma.



“Kule vijijini bado tuna shida ya wataalam hawatutembelei Wafugaji sasa kama Mkoa hembu hili jambo tulipe uzito tusiishie leo kwenye kongamano kwamba hawa watu wameonesha nia njema na ndio maana wanakuja wapate elimu, ujuzi na Tuwaunganish else vizuri maafisa ugani kwamaana ya Mifugo, Kilimo kwenda vijijini kuwatembelea Wafugaji na kuwapa elimu”.Amesema Megitii


Mwenyekiti huyo Amesema Wafugaji wa kuku wanapaswa kuongeza uzalishaji wenye tija Dodoma ili kujivunia uwepo wa makao makuu na kuwataka wataalam hao kuwapa elimu bora ya kufuga washiriki waliofika na kwamba wana nia njema ya kutambua mbinu za ufugaji bora ili waweze kupata tija nakuongeza mitaji Pamoja na uchumi wao.


Ametoa rai kwa wafugaji wa kuzingatia ulishaji na utunzaji wa chakula cha mifugo Pamoja na kuzingatia kanuni za magonjwa.


“Tunashindwa kufuga kwa tija kwasababu hatuzingatii kanuni za kiafya kwa maana ya ufugaji bora kwahiyo tukizingatia kuchanja kuku yaani kuchanja kinga ili wasipate maradhi ya kuambukiza alafu ukawapa maji ya kutosha Nina hakika tutabadilisha maisha na kuuza kuku kila siku.” Ametoa rai Megitii





Akifanya majumuisho baada ya kuzunga katika baadhi ya Mabanda amesema amefurahi kuona kikundi cha vijana wanufaika wa Mikoa ya vijana ya 4% ilivyoweza kubadilisha maisha ya vijana watano na kuajiri vijana wengine watano.


“hii inaonesha kuwa mafanikio kwa vijana ni makubwa na utayari wa vijana kujifunza ni mkubwa hivyo kinachobaki kwetu Viongozi ni kuhamasisha wananchi kukubali na kuanza kutumi bidhaa zetu”.Amefafanua Megitii

Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: