Mkuu wa Mkoa wa Lindi  Zainab Telack  amezindua rasmi Maonesho ya Madini na Uwekezaji.
Waziri Gao ni mmoja ya wachimbaji wa madini katika wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi



Na Fredy Mgunda,Iringa.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi  Zainab Telack  amezindua rasmi Maonesho ya Madini na Uwekezaji kwa lengo la kuongeza fursa za kiuchumi kwa wananchi wa mkoa huo


Telack amezindua maonesho hayo kwenye kikao cha wadau wa madini kilichofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mhe. Telack amesema kuwa Maonesho haya yanafanyika maalum Kwa ajili ya kutangaza fursa za madini zilizopo Mkoani Lindi ikiwemo dhahabu yenye ubora wa juu, graphite, gypsum, manganese,nickel, marble, Vito, Safaya na madini mengine isipokuwa Tanzanite na Almasi.

Telack ameongeza kuwa pamoja na uwepo wa fursa za madini, Mkoa wa Lindi una fursa za uwekezaji kwenye kilimo, fukwe nzuri za bahari, utalii, uchakataji wa mazao hasa korosho na ufuta.

Kupitia kikao hicho, Telack amewakaribisha wadau wote kwenye sekta ya biashara, Viwanda, madini na sekta zote za uchumi kushiriki kwenye Maonesho ya Madini na Uwekezaji yatakayofanyika Wilayani Ruangwa kuanzia tarehe 21-26 Agosti 2023.
Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: