Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakati wa mkutano wake na wanahabari kutolea ufafanuzi wa taarifa ya kwamba Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga -Bombo leo kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Japhet Simeo na wa kwanza kushoto ni Mratibu wa Kambi ya Upasuaji wa Kurekebisha Viungo (Plastic Surgery) kwenye Hospitali hiyo Dkt Wallace Karata

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakati wa mkutano wake na wanahabari kutolea ufafanuzi wa taarifa ya kwamba Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga -Bombo leo kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Japhet Simeo na wa kwanza kushoto ni Mratibu wa Kambi ya Upasuaji wa Kurekebisha Viungo (Plastic Surgery) kwenye Hospitali hiyo Dkt Wallace Karata na wa kwanza kulia ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga -Bombo Dkt Mohamed Saleh
Sehemu ya watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa tanga Bombo wakimsikiliza Waziri Ummy



Na Oscar Assenga, TANGA

SERIKALI imesema itakwenda kusaini makubaliano ya kuufanya mkoa wa Tanga kupitia Hospitali ya Rufaa ya Bombo kuwa kituo umahiri cha kufanya upasuaji wa kurekebisha viungo nchini.

Amesema urekebishaji huo wa viungo utakuwa ni kumrejesha mtu kwenye hali yake ya kawaida na hivyo kuwa cha kwanza kwa ukanda wa Afrika Mashariki.

Kauli hiyo ilitolewa leo na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakati wa mkutano wake na wanahabari kutolea ufafanuzi wa taarifa ya kwamba Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga -Bombo wanakwenda kurekebisha maumbile kulitokea maneno mengi.


Alisema lengo la upasuaji ni wa kumrekebisha mtanzania viungo vyake ili aweze kufanya kazi vizuri kwa niaba ya Serikali watashiriki Muhas, Wizara ya Afya ikiwemo Bombo na Hospitali ya Taifa Muhimbili na Interplastic na Chuo Kikuu cha Beirut cha Ujerumani ndio watashirikiana nao.

“Kubwa tunawashukuru wenzetu wa ujerumani kwa kurekebisha viungo vya watanzania waliopata changamoto mbalimbali ikiwemo ajali za moto wakiwemo Taasisi ya Taden kupata wadau hao Habibu Nuru na Dkt Ally fungo”Alisema

Alisema kwamba upasuaji huo ni sana hivyo alitoa wito kwa watanzania wawe na utamaduni wa kujitokeza kwenye maeneo mbalimbali wanapofanya kambi za matibabu,

“Taasisi ya Interplastic ya Ujerumani na tutafanya nao kazi na Chuo Kikuu cha Beiruti cha Ujerumani hivyo upasyuaji huu ni muhimu sana kwa Watanzania kubwa tunafurahia kumuona kijana wa kitanzania ambaye alilala miezi nane wenzao wamesaidia wamerekebisha viungo leo yupo nchini Ujerumani kwa niaba ya Serikali tunampenda kumshuuru Profesa Yugen Dog”Alisema

Hata hivyo alisema kwamba madaktari hao Bingwa wa kirekebisha viungo sita kutoka nchini ujerumani wapo Bombona Dkt Mohamed alinieleza zaidi ya watu 250 wameomba kufanyiwa upasuaji .

Waziri Ummy alimshukuru Profesa wa InterPlastic, Bombo na chuo Kikuu kishiriki Muhas kutoa kwa kutoa huduma kubwa ya upasuaji wa kurekebisha viungo ili kumrudisha mtu kwenye utendaji wake wa kawaida.

Awali akizungumza katika mkutano huo, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga -Bombo Dkt Mohamed Salehe alisema kwamba kambi hiyo wameshaianza walifanya uchunguzi kwa siku mbili na tarehe 27 mpaka 28 wamepanga kwa ajili ya upasuaji ,mpaka sasa watu walioandikiwa ni 250 na kati yao waliochunguzwa 196 na waliotayari kufanyiwa upausjai wagonjwa 86 ,na mpaka leo siku ya poili wagonjwa 18 wamekwisha kufanyiwa upasuaji.

Naye kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Japhet Simeo alisema wanashukuru Waziri Ummy kwa ujio wake kwa kuwaboreshea mazingira ya kazi na wanawatumishi wazuri na uongozi wa hospitali wapo vizuri.

Alisema huduma zinaotolewa kwa sasa urekebishaji viungo kumfanya mtu arudi kwenye ufanisi wa kawaida na zipo gharama ndogo ambazo wananchi wanachangia ambazo ni vipimo na utaratibu wa usajili ikiwemo wakati uendelezaji wa matibabu.

“Hivyo niwahakikishie huduma inayotolewa kwa mgonjwa mmoja ambayo ingeweza kutolewa zaidi ya milioni 1 hadi 2 hapa mteja mmoja haiwezi kuzidi 50,000 anachangia gharama kidogo.
Share To:

Post A Comment: