Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limeibuka kidedea na kutunukiwa Tuzo katika maonesho ya 10 ya  Biashara na Utalii yaliyofanyika jijini Tanga kuanzia Mei 28 hadi Juni  6, 2023.

Ushindi huo ambao TANAPA imeupata unatokana na kutoa elimu ya uhifadhi na utalii ikiwa ni huduma ambayo huitoa kwa watalii wa ndani na wa kimataifa ambao wameendeleo kuongezeka katika hifadhi za taifa.

 Tuzo hii imeliheshimisha shirika na kutoa hamasa ya kuendelea kutoa huduma bora na zenye viwango vya kimataifa.

TANAPA imepata tuzo hiyo kwa kunadi vyema  vivutio vyake vilivyomo katika hifadhi za taifa 22.

Maonesho haya ya Biashara na Utalii yaliyobebwa na kaulimbiu  "Kilimo, Viwanda, Utalii na Madini ndio msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi" yaliyoandaliwa na Tanzania Chamber of Commerce, hufanyika kila mwaka mkoani Tanga katika viwanja vya Mwahako  yakijumuisha makampuni, taasisi za serikali na zisizo za kiserikali. @tanzaniaparks 

Share To:

Post A Comment: