Wafanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD) wakiendelea na zoezi la kuhesabu malikatika maghara yao.
Na Dotto Mwaibale,
BOHARI ya Dawa (MSD) imeanza rasmi zoezi la kuhesabu mali kwa mujibu wa sheria. Zoezi hilo la kuhesabu mali linategemewa kukamilika mwishoni mwa mwezi Juni 2023 ili kuanza mwaka mpya wa fedha.
Katika kipindi hiki maghala yote ya MSD Makao Makuu pamoja na Kanda zote yatakuwa yamefungwa kupisha zoezi hilo.
Awali kabla ya
kuanza kwa zoezi hilo Bohari ya Dawa (MSD) iliwaarifu wateja wake wote wa
Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati kuwa kuanzia Juni 15, 2023 mpaka Juni 30, 2023
litafanyika zoezi la kuhesabu mali kwa mujibu wa sheria na kuwa kutokana na
zoezi hilo la kuhesabu mali, maghala yote ya MSD yatafungwa kwa kipindi cha
wiki mbili kuanzia Juni, 15, 2023.
Maombi yote ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara yawasilishwe MSD kabla ya Juni 7, 2023, ili kukidhi mahitaji wakati wote maghala hayo yatakapokuwa yamefungwa na kuwa huduma ya dharura ya kupata mahitaji itatolewa, pale tu itakapothibitika uhitaji.
Post A Comment: