Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa kiasi cha Shilingi Bilioni 12.3 kwa ajili ya miradi ya Maendeleo katika Wilaya ya Mpwapwa.

Senyemule ameyasema hayo leo Juni 15, 2023 Wilayani Mpwapwa wakati akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya Mkoa wa Dodoma mbele ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Bw. Daniel Chongolo ambae ameanza ziara ya kikazi ya siku 10 Mkoani Dodoma.

Ameitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na ujenzi wa Shule za Msingi na Sekondari, madarasa, Maabara, Vituo vya Afya, Zahanati na miundombinu ya barabara.

Senyamule amesema Mkoa wa Dodoma unajivunia mafanikio makubwa yaliyopatikana hususan katika ujenzi wa Shule na madarasa na kutoa rai kwa wazazi kuhakikisha watoto wote wanapelekwa shule.

"Sote ni mashahidi Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya makubwa kwenye elimu tuhakikishe watoto wetu wanaenda Shule kusiwe na vikwazo vyovyote. Huduma ya maji, umeme na Afya kote huko mageuzi makubwa yamefanyika chini ya Serikali ya Awamu ya Sita" Amesema Senyamule

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Bw. Daniel Chongolo ameanza ziara ya kikazi Mkoa wa Dodoma kwa siku 10 kwa lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo leo hii amekagua miradi ya maji na kuchangia mifuko 100 ya saruji ili kukamilisha ujenzi wa zahanati ya Kimagai.

Share To:

Post A Comment: